Monday, December 30, 2013
Saturday, December 28, 2013
Mbeya jiji yapeta matokea darasa la saba..Ileje yashika mkia kimkoa.
HALMASHAURI ya jiji la Mbeya imeshika nafasi ya kwanza kimkoa kwa shule zake za msingi kufanya vizuri katika matokeo ya wahitimu wa elimu ya msingi mwaka huu huku wilaya ya Ileje ikishika mkia kwa kushika nafasi ya kumi.
Hsalmashauri ya jiji imeongoza kimkoa kwa kupata wastani wa asilimia 65.5 ikafuatiwa na Rungwe yenye wastani wa 50.9,Wilaya ya Kyela imeshika nafasi ya tatu kwa wastani wa 46.4 huku wilaya ya Mbarali ikishika nafasi ya nne kwa wastani wa 43.6.
Halmashauri ya Mbozi inashika nafasi ya tano ikiwa na wastani wa 42.8,Busokelo ikiwa ni halmashauri mpya inashika nafasi ya sita kwa wastani wa asilimia 42.7,Momba ikiwa ni halmashauri mpya pia ikashika nafasi ya saba kwa wastani wa asilimia 36.3.
Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imeshika nafasi ya nane kwa wastani wa 35.6,nafasi ya tisa ikaangukia kwa wilaya yenye eneo kubwa sawa na asilimia 47 ya eneo lote la mkoa wa Mbeya wilaya ya Chunya iliyopata wastani wa asilimia 32.4 na Ileje ikashika mkia kwa kupata asilimia 30.8 ya ufaulu.
Akitangaza matokeo kwa ujumla kwenye kikao cha Bodi cha Bodi ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza,afisa elimu mkoa wa Mbeya Remigius Ntyama alisema katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kiwango cha ufaulu kimeshuka ikilinganishwa na malengo ya kitaifa.
Ntyama alisema mwaka 2011 kiwango cha ufaulu kimkoa kilikuwa asilimia 55,mwaka 2012 kikawa asilimia 30 na mwaka huu yamepanda kidogo kwa kufikia asilimia 44 japo hayajafikia malengo ya kitaifa ya asilimia 60 ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.
Akifafanua zaidi juu ya matokeo ya mwaka huu afisa elimu huyo alisema waliofanya mtihani walikuwa 65,484 kati yao wakiwamo wavulana 30,367 na wasichana 35,117.
Alisema waliofaulu kwa wastani wa kati ya alama 100 na 250 ni wahitimu 29,065 sawa na asilimia 44.38 ya waliofanya mtihani wakiwemo wavulana 14,246 na wasichana 14,419.
Waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kulingana na vyumba vya madarasa vilivyopo ni 27,581 sawa na asilimia 94.89 kati yao wakiwemo wavulana 13,528 na wasichana 14,053 wakati waliosalia watachaguliwa baada ya mahitaji ya vyumba 59 kukamilishwa ambapo halmashauri ya jiji la Mbeya inaongoza kwa kuwa na uhaba wa vyumba 44 vya madarasa.
Akizungumza wakati wa kufungua na pia kufunga kikao hicho,kaimu katibu tawala mkoa wa Mbeya Leonard Magacha aliwasisitiza wajumbe kutambua kuwa kila mmoja anayo nafasi ya kuhakikisha changamoto za elimu zinapatiwa ufumbuzi kwenye eneo lake.
Friday, December 27, 2013
Wanahabari wakiwa katika kubadilishana mawazo ya mwisho wa mwaka walipokutana na mhariri wa Lyamba Lya Mfipa.
Tuesday, December 24, 2013
MBARALI WANAHITAJI ELIMU YA UFUGAJI BORA WA NGURUWE
Saturday, December 21, 2013
MADIWANI WATAKA TAARIFA YA MAUZO YA JEZI ZA MBEYA CITY
Friday, December 20, 2013
MAUAJI YA KUTISHA YAFANYIKA NYUMBANI KWA DIWANI WA CCM
MAUAJI ya kinyama yamefanyika nyumbani kwa diwani wa kata ya Nkangamo wilayani Momba(CCM) baada ya mwanaye na mfanyakazi wa ndani kuuawa kikatili na watu wasiofahamika.
Diwani aliyekumbwa na maswahibu hayo ametajwa kwa jina la Eston Kimwelu(55) mkazi wa mtaa wa Tazara katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba ambapo mauaji hayo yalitokea Desemba 19 mwaka huu saa 8:00 mchana nyumbani kwake.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki amewataja waliouawa katika tukio hilo kuwa ni mtoto wa diwani huyo Kalibu Kimwelu(6) aliyeuawa kwa kuchinjwa shingo kwa kisu wakati mfanyakazi wa ndani Sista Nyilenda(17) aliuawa kwa kunyongwa shingo kwa kutumia waya wa Luninga uliopo katika sebule ya nyumba ya familia hiyo.
Masaki amesema wakati mauaji hayo yakitokea diwani Kimwelu alikuwa shambani kwake katika kijiji cha Kipaka huku mkewe Tumaini Yohana(29) katibu muhtasi wa halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma wilayani hapa akiwa kazini.
Amesema miili ya marehemu wote wawili ilikutwa katika sebule ya nyumba hiyo lakini pia bada ya kuchunguza ikabainika wauaji waliiba mabegi mawili yenye nguo yaliyokuwa katika chumba wanacholala watoto.
Kaimu kamanda huyo amesema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa ijapokuwa kinahusisha na mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia baina ya mke mdogo na mkubwa ambapo familia ya mke mkubwa imekuwa ikidai kutelekezwa na mumewe kwa kunyimwa mali yakiwemo mashamba.
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia watu watano wakiwemo watoto watatu wa mke mkubwa aliowataja kwa majina ya Enock(23) ,Gabriel(19) na Alex(16) na marafiki wa familia hiyo Mussa Ngoba(19) na Patrick Msigwa(18).
MADIWANI WA CHADEMA WADAIWA KUTISHIA MAISHA YA MEYA
Thursday, December 19, 2013
MAAFA YA KIMBUNGA CHA MVUA YENYE UPEPO MKALI YALIVYOITIKISA MBARALI.MKUU WA MKOA WA MBEYA AFANYA ZIARA KUWAFARIJI WAATHIRIKA.
Wednesday, December 18, 2013
MIUNDOMBINU DUNI YA SOKO BADO NI TATIZO KWA MATUNDA YANAYOZALISHWA KATIKA KATA YA KIWIRA WILAYANI RUNGWE
MFANYABIASHARA TUNDUMA AJERUHIWA KWA RISASI NA MAPANGA KISHA KUPORWA MAMILIONI
Polisi mkoani Mbeya inawasaka watu wanne wasiofahamika kufuatia watu hao kumvamia mfanya biashara ya kubadilisha fedha na kumjeruhi kwa risasi na mapanga na kisha kumpora fedha.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki alimtaja mfanyabiashara aliyevamiwa kuwa ni Alphonce Mwanjela(36) mkazi wa eneo la Sogea Makambini katika mji mdogo wa Tunduma uliopo wilayani Momba.
Masaki alisema tukio hilo limetokea Desemba 16 majira ya saa 1:45 ya usiku katikika eneo la Sogea Makambini umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwa mfanyabiashara huyo wa kubadili fedha ambaye hufanya shughuli zake katika mpaka wa kati ya Tanzania na Zambia..
Amesema akiwa anarudi nyumbani kutoka kazini, Mwanjela aliyekuwa amebeba fedha alivamiwa na kundi la watu wanne wasiofahamika na ndipo wakaanza kumjeruhi kwa kumkata mapanga kichwani na pia kumjeruhi kwa kumpiga risasi mguu wake wa kulia wakitumia bunduki inayodhaniwa kuwa ya aina ya ni Short Gun.
Amesema baada ya kumjeruhi watu wao walimnyang’anya mfanyabiashara huyo fedha taslimu kiasi cha shilingi 5,200,000 fedha za kitanzania,dola 2,300 za kimarekani na Randi 10,000 za Afrika ya kusini.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda huyo,majeruhi alikimbizwa na wasamaria wema katika kituo cha afya cha Tunduma alikolazimika kulazwa na afya yake imetajwa kuendelea vizuri.
Kufuatia tukio hilo,Masaki amesema msako mkali unaendeshwa na jeshi la polisi ili kuwabaini watu waliohusika na kutoa wito kwa watu au mtu yeyote aliye na taarifa juu ya mahali waliko kutoa taarifa katika mamlaka yoyote iliyopo jirani ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amewataka pia wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara ya kubadili fedha katika mpaka wa Tunduma kuungana pamoja na kufungua duka la kubadili fedha litakalosajiriwa na kuweza kupewa ulinzi mzuri badala ya kuendelea kufanya shughuli hiyo kiholela na kuhatarisha maisha yao.
Amewataka pia watu wanaotaka kubadili fedha zao kwenda katika tasisi zilizo rasmi akisema pia si rahisi kuweza kutapeliwa kama inavyofanyika kwa wale wanaokwenda kubadili kwa wafanyabiashara wasio rasmi wanaowakuta barabarani.
MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI AFA MAJI AKIOGELEA MTO CHUNYA
MVUA zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani hapa zimeendelea kuleta maafa kwa kuwezesha mito kujaa maji na kusababisha vifo vya watoto wanaoogelea.
Ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu mtoto mmoja aripotiwe kufa maji huko wilayani Mbarali alipokuwa akiogelea mtoni na wenzake,jeshi la polisi mkoani hapa limesema mtoto mwingine amekufa maji wilayani Chunya.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki amesema leo kuwa aliyekufa maji ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Chokaa wilayani Chunya aliyemtaja kwa jina la Ezekia Azigeti(10).
Kamanda Masaki amesema mwanafunzi huyo alipoteza maisha Desemba 16 mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni baada ya kuzidiwa na maji alipokuwa akiogelea katika mto Chunya.
Aidha kaimu kamanda huyo ametoa wito kwa wazazi na walezi wa watoto mkoani Mbeya kuwa makini na watoto wao katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha kwa kuwakanya kwenda kuoga katika mito,mabawa au madimbwi ya maji.
Amewataka pia wakazi kuhakikisha wanachukua tahadhari kwa kufukia au kufunika na kuziba mashimo na visima vilivyo wazi ili kuepusha vifo vya watoto vitokanavyo na maji.
Sunday, December 15, 2013
WADAU WAJITOKEZA KUSHIRIKI KAMPENI YA SHARING IS MORE THAN GIVING
Subscribe to:
Comments (Atom)

