SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limepanga mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya CRDB Federation Cup kati ya bingwa mtetezi Yanga SC dhidi ya JKT Tanzania kufanyika katika dimba la CCM Mkwakwani Jijini Tanga.
Nusu fainali nyingine imepangwa kuchezwa katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa Manyara ikiwakutanisha Simba SC dhidi ya Singida Black Stars.
Michezo hiyo ya
kuwatafuta wanafainali wa Federation Cup 2024-2025 imepangwa kufanyika kati ya
Mei 16-18, 2025.

No comments:
Post a Comment