Friday, August 23, 2013
I LOVE MBEYA CITY
MAANDALIZI MASHINDANO YA CHANETA TAIFA NDANI YA UWANJA WA SOKOINE JIONI HII
Wednesday, August 21, 2013
MAANDALIZI YA LIGI KUU TANZANIA BARA NDANI YA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA
MAANDALIZI YA MICHUANO YA CHANETA TAIFA ITAKAYOFANYIKA JIJINI MBEYA
Monday, August 19, 2013
KANDORO MGENI RASMI MKUTANO WA JUMUIYA YA AHMADIYYA KESHO MBEYA
Thursday, August 15, 2013
MTANDAO WIZI WA BODA BODA WANASWA.WATUMIA SARE ZA JWTZ
MNAMO TAREHE 14.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:50HRS HUKO AIRPORT - TANKINI JIJI NA MKOA WA MBEYA. DANIEL S/O SONGELA, MIAKA 24, KYUSA, DEREVA WA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA ZZK-MBALIZI, ALINYANG’ANYWA PIKIPIKI YAKE T.691 CJF AINA YA KINGLION NA WATU WAWILI. MBINU NI KUKODIWA NA MTEJA MMOJA KWA UJIRA WA TSHS 5,000/= KUTOKA MBALIZI HADI ENEO LA ESSO NA NJIANI WALIKUTANA NA MTU MWINGINE ALIYEVAA SARE ZA JWTZ AKIWA AMESHIKA PANGA HIVYO WALIFANIKIWA KUMPORA MHANGA PIKIPIKI HIYO. KUFUATIA TUKIO HILO JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WAENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA LILIFANYA MSAKO NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WAWILI 1. BARAKA S/O DAUDI, MIAKA 20, KYUSA, BIASHARA MKAZI WA MAMA JOHN NA 2.SHADRACK S/O ESSAU, MIAKA 21, BIASHARA , MKAZI WA MWAMBENE WAMEKAMATWA NA KUKIRI KUHUSIKA KATIKA MATUKIO YA UPORAJI WA PIKIPIKI MAENEO MBALIMBALI. JUMLA YA PIKIPIKI NANE ZINAZODHANIWA KUWA MALI YA WIZI ZIMEKAMATWA KATIKA MSAKO HUKO TUKUYU WILAYA YA RUNGWE NA WATUHUMIWA SITA WAMEKAMATWA 1.SIMON S/O MWANYASI, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA 2.LWITIKO S/O HADSON, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA 3. OSFA S/O MWAMAKULA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA 4.FESTO S/O GIDEON, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA 5.SOFIA D/O GIDEON, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA NA 6.NOEL S/O YESAYA, MIAKA 34, KYUSA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA TUKUYU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIPATIA KIPATO / MALI KWA NJIA YA MKATO KWA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE NA SHUGHULI HALALI ZA KUJIPATIA KIPATO. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WALIOWAHI KUIBIWA AU KUPOTELEWA PIKIPIKI ZAO KUFIKA KITUO CHA POLISI KATI MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MALI ZAO.
Wednesday, August 14, 2013
AUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO NA MPENZI WAKE
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 00:05 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. MARIA D/O MARTIN, MIAKA 37, MNYAMWEZI, MKULIMA, MKAZI WA KANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI KICHWANI NA KUKABWA SHINGONI NA MPENZI WAKE AITWAE LAMECK S/O MSANGAWALE, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KANGA. CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MWANAUME MWINGINE. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUYATATUA MATATIZO YAO YA KIJAMII KWA NJIA YA MEZA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA. PIA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 07:00 HRS UKO KIJIJI CHA NANSAMA KATA YA ISANSA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. SIJAONA S/O HAONGA MIAKA 45, MKULIMA, MNYIHA, MKAZI WA NANSAMA ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KUTUPWA KATIKA MTO MLOWO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI MGOGORO WA MASHAMBA KATI YA MAREHEMU NA SHABANI S/O MBWILI PAMOJA NA MAWAZO S/O MBWILI AMBAO WALITOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO. MAREHEMU ALIVIZIWA WAKATI AKIVUA SAMAKI NA PEMBENI YA MWILI WAKE KULIKUTWA NDOANO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO NA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
Tuesday, August 13, 2013
WATATU WAFA KATIKA MATUKIO TOFAUTI
WATU watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya, katika matukio mawili tofauti likiwemo la wachungaji wa mifugo kumuua mvuvi mmoja.
Tukio la mauaji ya mvuvi, lilitokea juzi katika Kijiji cha Itindi wilayani Chunya.
Mvuvi aliyeuawa alitajwa kwa jina la Hatibu Mwakalinga(36), ambaye aliuawa kwa kupigwa na fimbo mbavuni na wachunga Ng’ombe wafugaji wa kabila la kisukuma.
Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa na kundi la Sungusungu wakikamata mifugo mali ya wafugaji waliofahamika kwa jina mojamoja la Mwanahela, Kabahungu na Lukangila.
Tukio la pili lilitokea jana katika Kijiji cha Mshewe kata ya Utengule Usongwe wilaya ya Mbeya Vijijini, ambapo watoto wawili walikufa kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuungua.
Waliofariki dunia ni Desmos Raphael(2) na Dorcas Raphael mwenye umri wa miezi minne.
Chanzo cha tukio hilo ni baada ya mama mzazi wa watoto hao Floiza Emmanuel(20), ambaye alikuwa amelala na watoto wake, kisha kutoka nje majira ya saa sita usiku kujisaidia na kuacha amewasha kibatari, na aliporudi akakuta nyumba yake inawaka moto.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote mawili na ametoa wito kwa wachunga mifugo waliosababisha kifo cha mvuvi wilayani Chunya kujisalimisha.
Sunday, August 11, 2013
AUA MKEWE KWA KUMNYONGA SHINGO.KISA WIVU WA MAPENZI
POLISI mkoani Meya inamshikila mkazi wa kijiji cha Mapogoro kata ya Miombweni wilayani Mbarali kwa tuhuma za mauaji ya mkewe kutokana na wivu wa mapenzi.
Anayeshikiliwa na jeshi hilo amefahamika kwa jina la Nkuva Malale(39) ambapo inadaiwa kuwa alimuua mkewe kwa kumpiga fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo maeneo ya kichwani kabla ya kumnyonga shingo.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman jana aliwaambia wandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea agosti 10 mwaka huu majira ya saa 10:30 kijijini Mapogoro.
Kamanda Athuman alimtaja aliyeuawa katika tukio hilo la kinyama kuwa ni Mbuke Ochegeri(34) aliyekuwa mkulima na mkazi wa kijiji hicho.
Alisema kabla ya kumshushia kipigo na kisha kumuua mtuhumiwa wa mauaji alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.
Aidha alisema uchughuzi zaidi juu ya mauaji hayo unaendelea na kubainisha kuwa wakati wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
CRDB WALIPOPANDA MITI NA KUKARABATI JENGO LA WODI YA WANAWAKE KATIKA HOSPITALI YA META MBEYA
MBEYA CITY YATANGAZA JEZI MPYA ZA MASHABIKI
Friday, August 9, 2013
PSPF YAKUTANA NA WADAU MKOANI MBEYA
Subscribe to:
Comments (Atom)