MNAMO TAREHE 27.02.2014 MAJIRA YA SAA 01:55HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. TITO HANKUGWE (45) KAIMU VEO WA KIJIJI CHA SHASYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI WAKATI ANATOA MSAADA NYUMBANI KWA FURAHA HANKUGWE AMBAYE ALIVAMIWA NA KUNDI LA WATU NANE NA KUBOMOLEWA NYUMBA YAKE PAMOJA NA KAKA YAKE SIKUJUA HANKUGWE TAREHE 26.02.2014 MAJIRA YA SAA 21:45HRS KATIKA KIJIJI CHA SHASYA, KATA YA HALUNGU, TARAFA YA ITAKA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI WA SOLA NA INVETA AMBAPO FURAHA HANKUGWE ALITUHUMIWA KUIBA NYUMBANI KWA MAPINDUZI MAGWAZA MKAZI WA KIJIJI CHA SHASYA. WATUHUMIWA HAO AMBAO WOTE WANAFAHAMIKA WAKIONGOZWA NA AMANI MAGWAZA – MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA NAMKWENDE, WENGINE NI MASHAKA BOKO, GIVEN MYOMBE, MAWAZO MAGWAZA, YOHANA MAGWAZA, TULINAO NZOWA, KENETH NGOYA, SIKUJUA NZOWA AMBAO WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA HAO ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki
Friday, February 28, 2014
KAIMU AFISA MTENDAJI WA KIJIJI AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI

Thursday, February 27, 2014
Wednesday, February 26, 2014
ZIARA YA RC KANDORO WILAYANI MBARALI
Wednesday, February 19, 2014
BIG RESULTS NOW(BRN) KATIKA KILIMO CHUNYA
Sunday, February 16, 2014
SIMBA YAIPIKU YANGA MAPATO NYUMBANI KWA MBEYA CITY

TUNDUMA WABOMOA KINGO ZA BARABARA MPYA YA LAMI KUIBA KOKOTO
SERIKALI mkoani Mbeya imeagiza kukamatwa mara moja kwa mtu yeyote atakayebainika kukusanya kokoto na mchanga pembezoni mwa barabara mpya iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka mji mdogo wa Tunduma kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ametoa agizo hilo jana baada ya kubaini uwepo wa baadhi ya wakazi katika mji wa Tunduma ambao wamekuwa wakitumia zana mbalimbali kubomoa barabara na kisha kuiba kokoto hivyo kuhatarisha uimara wa barabara hiyo iliyojengwa hivi karibuni.
Akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Momba,Kandoro ameshuhudia uharibifu huo wa barabara pasipo uoga baadhi ya wakazi wamekutwa wakikusanya kokoto hizo na kuzirundika pembezoni mwa baarabara wakisubiri wateja.
Meneja mradi wa mradi wa barabara hiyo kutoka wakala wa Barabara(Tanroads) Eliazary Rweikiza alisema takribani kilometa tano za kipande cha barabara hiyo zimeathiriwa na wizi huo unaohatarisha uimara wa barabara.
Akizungumzia uharibifu huo,mkuu wa mkoa aliyeonekana kukasirishwa na vitendo hivyo,ameamuru kukamatwa mara moja kwa wezi hao pamoja na wateja wanaonunua kokoto zilizoibwa na kufikishwa katika mikono ya sheria.
Alisema lengo la serikali kuwekeza mamilioni ya fedha katika miundombinu ya barabara ni kurahisisha mawasiliano kupitia njia hiyo ili maendeleo yaweze kupatikana kwa urahisi hivyo haivumiliki kuona watu wachache wakikwamisha jitihada hizo.
Wednesday, February 12, 2014
MAISHA HAYA MPAKA LINI?
Saturday, February 8, 2014
WANAWAKE WAUAWA NA WAUME ZAO KISA WIVU
VIJANA MATATANI KWA NOTI BANDIA
Tuesday, February 4, 2014
ZIARA YA RC KANDORO SIKU YA KWANZA MBEYA VIJIJINI
Subscribe to:
Comments (Atom)