Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, June 30, 2024

JE NI KWELI YANGA YA SASA HAIACHI KOMBE?


Unaambiwa ukianzisha kombe lolote waambie Yanga.

Full Time — Safari Champions 1 - 4 Yanga SC.
⚽️ Omary Mfaume
⚽️ Shekhan
⚽️ Prosper
⚽️ Hussein
ℹ️ Safari lager FC ni timu iliyoundwa baada ya kutafutwa kwa vipaji katika mikoa minne ambayo ni Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.

Mchujo ulianza tangu mwaka jana (2023) chini ya Makocha Sekirojo Chambua, Jamhuri Kihwelo 'Julio' na Alberto Pereira.
Idadi ya wachezaji kila Mkoa :
◉ 8 - Mbeya.
◉ 4 - Mwanza.
◉ 5 - Dar es Salaam.
◉ 5 - Arusha.
Note : Haya ni sehemu ya maandalizi ya kujenga kikosi imara cha baadae cha timu ya Taifa "Taifa Stars"

YANGA BINGWA SAFARI LAGER CUP

 




Vijana wa Yanga jana walibeba taji la Safari Lager Cup baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Safari Champions.

Full Time
Safari Champions 1-4 Yanga
Shekhan⚽
Omary Mfaume⚽
Prosper⚽
Hussein⚽

Wednesday, June 26, 2024

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA WILAYA YA KYELA


 

CHUNYA WAJIZATITI KEN GOLD KUCHEZA NYUMBANI LIGI KUU

 


Na Mwandishi Wetu, Chunya.

 

HALIMASHAURI ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imewahakikishia wapenzi wa soka kuwa michezo ya Timu ya Ken Gold iliyopanda ligi kuu wataishuhudia kwenye uwanja uliopo  wilayani hapa kwakuwa mikakati imewekwa kuhakikisha ujenzi wa uwanja huo unakamilika kwa wakati.

 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Chunya, Tamim Kambona tayari Shilingi milioni 200 imeytengwa na halimashauri hiyo kwaajili ya muendelezo wa ujenzi wa uwanja huo wa michezo uliopo katika Kata ya Mbugani.

 

Akizungumza na mwandishi wetu, Kambona alisema lengo la halimashauri ni kuona mradi wa ujenzi wa uwanja wa michezo uliopo Kata ya Mbugani unaomilikiwa na Halmashauri hiyo unakamilika kwa wakati kabla ya kuanza kwa ligi Kuu mwaka 2024/2025.

 

Alisema wanao uhakika Ken Gold itautumia uwanja huo kwa mechi zake za nyumbani kwakuwa mbali ya kutenga fedha hiyo kupitia mapato yake ya ndani pia imeunda Kamati maalumu ya wadau inayoongozwa na Ayoub Omary ili kusimamia kwa karibu mradi huo.

 

Kambona alisema sanjari na mipango ya Kamati Halmashauri inatarajia kutenga fedha nyingi zaidi mwaka ujao wa fedha ili kuuboresha zaidi uwanja huo na kuwa wa kisasa kwa kuwekwa nyasi bandia.

 

Mkurugenzi huyo pia aliwashukuru wadau wanaoendelea kutoa michango ya hali na mali akiwemo mwekezaji kwenye Sekta ya Madini aliyemtaja kwa jina la David Mathayo aliyesema ametoa tingatinga kwa ajili ya kushindilia uwanja.

 

Aliwataka wadau wengine kuunga juhudi zinazofanywa na halimashauri ili kuhakikisha uwanja unakamilika kabla ya mashindano ambapo wananchi wataongeza mapato yao kutokana na ujio wa wageni kutoka nje ya Wilaya na Mkoa kwa ujumla.

 

Mmoja wa wafanyabiashara na mkazi wa Kata ya Chokaa wilayani hapa, Boniphace Mwinuka alisema hatua ya kupanda daraja kwa timu ya Ken Gold inaleta hamasa kubwa ya michezo katika Wilaya ya Chunya kwani wengi wa wakazi walikuwa wakisafiri kwenda jijini Mbeya ili kushuhudia michezo ya ligi kuu.

 

Mwinuka alisema miongoni mwa faida zitakazopatikana kwa wakazi wilayani hapa iwapo ligi kuu itacheza kwenye uwanja huo ni pamoja na wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni kupokea wageni wengi pamoja na wajasiriamali na madereva wa Bodaboda kusafirisha abiria kutoka maeneo mbalimbali.

Wednesday, June 5, 2024

𝐊𝐈𝐊𝐎𝐒𝐈 𝐁𝐎𝐑𝐀 𝐂𝐇𝐀 𝐅𝐄𝐈𝐒𝐀𝐋 2023-2024

 

Kiungo wa Azam FC Feisal Salum Ameorodhesha Kikosi chake Bora Msimu huu 2023/24 akihojiwa na Televisheni Fulani Nchini.

Katika Kikosi hicho :-
🇲🇱 Djigui Diarra __ Young Africans
🇨🇮 Koussi yao __ Young Africans
🇹🇿 Pascal Msindo __ Azam FC
🇹🇿 Ibrahim Bacca __ Young Africans
🇨🇴 Fuentes Mendoza ___ Azam FC
🇺🇬 Khalid Aucho ___ Young Africans
🇨🇮 Pacome Zouazoa __Young Africans
🇹🇿 Mudathiri Yahya ___ Young Africans
🇨🇮 Joseph Guede ___ Young Africans
🇹🇿 Feisal Salum ___ Azam FC
🇧🇫 Stephen Azizi Ki ___ Young Africans
Wachezaji Nane (😎 Kutoka Yanga na Wachezaji (3) Kutoka Klabu ya Azam FC ndiyo Wameunda Kikosi cha Feisal Salum cha Msimu huu 2023-2024.