Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya Tamasha la Kuibua vipaji.
Tamasha la kuibua vipaji vya kucheza(Dance),mitindo(Fashion),kuchekesha(Comedy)
na Dj Mixing lililoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust litafanyika Oktoba
25-28,2024 katika uwanja wa Chuo cha Uhasibu(TIA) jijini Mbeya.
Akitoa taarifa kwa wanahabari Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo amesema tamasha hilo ni la tano kufanyika ambalo litajumuisha washiriki kutoka nchi nzima.
“Fomu zimeanza kutolewa Oktoba 9,2024 hadi Oktoba 20,2024 saa 9:30 alasili katika ofisi za Tulia Trust zilizopo Uyole jijini Mbeya, Tukuyu wilayani Rungwe na Kyela.
Sifa za mshiriki awe ni Mtanzania yeyote mwenye kipaji Mawasiliano namba 0657389521 na 0769060738.
Mshindi wa kuimba atarekodi nyimbo katika studio ya
Black Dot Music iliyopo Jijini Dar es Salaam.




