Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, May 15, 2025

HUYU HAPA MWAMUZI MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO


 Baada ya kuthibitishwa kwa uwanja wa mechi, Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza uteuzi rasmi wa waamuzi kwa fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.

CAF imemteua mwamuzi wa kimataifa kutoka Mauritania, Dahane Beida, kuwa mwamuzi wa kati katika mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF kati ya Simba SC ya Tanzania na RS Berkane ya Morocco. Mchezo huo umepangwa kufanyika tarehe 25 Mei 2025 katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Dahane Beida ni mwamuzi mwenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika. Miongoni mwa mechi kubwa alizowahi kuzisimamia ni fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023 kati ya Ivory Coast na Nigeria. Pia, alisimamia mechi ya marudiano ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2022/23.
Fainali ya mwaka huu inatarajiwa kuwa ya kusisimua, kwani Simba SC itakuwa inacheza fainali yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho, huku RS Berkane wakitafuta taji lao la tatu katika mashindano haya, baada ya kulibeba mwaka 2020 na 2022.
Mchezo wa kwanza wa fainali hiyo utafanyika tarehe 17 Mei 2025 katika Uwanja wa Berkane Municipal, Morocco.

Saturday, April 19, 2025

MRATIBU MISS TANZANIA AFARIKI DUNIA

 


Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania Hashim Lundega, amefariki dunia leo Jijini Dar es Salaam.

Lundenga ambaye ameugua kwa muda mrefu itakumbukwa ndio aliyesimamia kwa mafanikio makubwa Mashindano ya Urembo Tanzania na kuyapa umaarufu mashindano hayo.

Lundenga pia aliwahi kuhudumu kwenye Kamati ndani ya Klabu ya Yanga.

Thursday, April 17, 2025

SIMBA YALAMBA MKATABA MNONO

 


Mkataba Wa Simba Sports Club Na JayRutty ni wa Shilingi Bilioni 38 kwa miaka mitano.

Kuna gawiwo la 5.6 Bilioni kila mwaka na ongezeko la asilimia 10 kwa kila mwaka 

FAIDA ZA KIMKATABA.

1. Ujenzi wa Uwanja wa Bunju (Watu Elf10 hadi 12).

2. Gari la IRIZAR .

3. Media production.

4. Ujenzi wa Ofisi Mpya

5. Kukuza Vipaji ( pesa cash kutolewa)

6. Pre seasons sponsorship

7. Medica room

8. Simba Day ( pesa itatolewa cash m100)

9. Motisha kwa wachezaji ( M470 cash)

10. Jezi za brand kubwa dunia

YANGA TANGA,SIMBA MANYARA



SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limepanga mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya CRDB Federation Cup kati ya bingwa mtetezi Yanga SC dhidi ya JKT Tanzania kufanyika katika dimba la CCM Mkwakwani Jijini Tanga.

Nusu fainali nyingine imepangwa kuchezwa katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa Manyara ikiwakutanisha Simba SC dhidi ya Singida Black Stars. 

Michezo hiyo ya kuwatafuta wanafainali wa Federation Cup 2024-2025 imepangwa kufanyika kati ya Mei 16-18, 2025.

Tuesday, April 8, 2025

ARSENAL KUIVAA REAL MADRID USIKU WA LEO UEFA

 

Klabu ya Arsenal ya Uingereza, usiku wa leo inawakaribisha mabingwa mara 15 wa Ulaya, Real Madrid katika mechi ya kwanza ya hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), katika mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Emirates, jijini London.

Timu hizo zilikutana kwa mara ya mwisho kwenye msimu wa UEFA 2005/06, ambapo ‘The Gunners’ ilisonga mbele kuelekea hatua ya robo fainali kwa ushindi wa wa 1-0 dhidi ya Real Madrid.
Je, Arsenal itafanya maajabu leo mbele ya mabingwa hao wa kihistoria wa Ulaya?