WANAWAKE wajawazito wanaopata huduma zao katika kituo cha afya cha Kirando wilayani hapa wanalazimika kujifungulia gizani kufuatia uhaba wa mafuta kwaajili ya jenereta unaokikabili kituo hicho.
Hali hiyo inatokana na kila mjamzito ama mgonjwa yeyote anayelazwa katika kituo hicho ambacho wakazi wa vijiji vilivyopo pembezoni na ndani ya ziwa Tanganyika wanakiona kama hospitali ndogo kutakiwa kwenda na vibatali,karabai ama taa ya mafuta kutoka majumbani mwao.
Iwapo mgonjwa aliyelazwa kituoni hapo atakosa uwezo kabisa wa kuja na kibatari,karabai ama taa basi hulazimika kukaa gizani usiku kucha iwapo katika wodi alimolazwa hakutakuwa na mgonjwa mwingine anayetoka kwenye familia iliyo na unafuu wa kiuchumi.
Uchunguzi wa kina wa Lyamba Lya Mfipa pia umebaini hali kuwa mbaya kwa wagonjwa hususani wajawazito wanaokwenda hapo na kutakiwa kufanyiwa upasuaji ambapo pia hutakiwa kununua mafuta ya jenereta ndipo wahudumiwe na iwapo watakosa basi huwa na wakati mgumu iwapo hawatojitokeza wasamalia wema kuwachangia.
KWA MWENDELEZO WA HABARI HII ENDELEA KUTEMBELEA Lyamba Lya Mfipa ..............
No comments:
Post a Comment