ASKARI Polisi wilayani Momba mkoani Mbeya wamefanikiwa kumnusuru
Mkuu wa wilaya hiyo Abiud Saudea na jopo lake baada ya kuzingilwa na wananchi
wa Kijiji cha Kamsamba.
Hali hiyo iliwakera wananchi na kuanza kuzomea jambo ambalo
lilizusha vurugu mbele ya Mkuu huyo wa wilaya, kamanda wa polisi wa wilaya hiyo
(OCD) na viongozi wengine.
Kutokana na fujo hizo, askari polisi waliingilia kati na
kuwatawanya wnanchi na mabomu ya machozi hali ambayo haikufua dafu na kuamua
kutumia risasi za moto ambazo zimejeruhi watu watatu ambao wamekimbizwa Hospitali
ya wilaya ya Mbozi mkoani hapa.
Mbali na hao watu wanne wamekamatwa kwa kuhusika na uratibu wa
fujo hizo wakiwemo viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) katika kata na kijiji hicho cha Kamsamba.
Waliokamatwa na Polisi ni pamoja na Richard Nyoni, Michael
Simfukwe ambao ni viongozi wa Chadema. Wengine ni Jofrey Dismas na Sabati
Kigaya.
No comments:
Post a Comment