POLISI mkoani Mbeya inamshikilia mkazi wa mtaa wa
Pambogo maeneo ya Airport Jijini Mbeya kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya
Short Gun na risasi saba alizokuwa akizimiliki kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi,amemtaja
anayeshikiliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni Emmanuel Mwakeja(27).
Kwa mujibu wa kamanda Msangi kijana Emmanuel
amekamatwa Oktoba 26 mwaka huu majira ya saa 12:40 jioni akiwa nyumbani kwake
Pambogo.
Kamanda Msangi alisema awali siku hiyo mnamo majira
ya saa 11 jioni maeneo ya uwanja wa Sokoine katika kata ya Sisimba mkazi wa
vMakunguru jijini hapa Alfonce Mwakasege(38) aligundua kuibiwa pikipiki yake
aina ya Kinglion yenye namba za usajiri T 683 BDM.
Amesema baada ya kufanyika kwa msako wa haraka juu
ya wizi wa pikipiki hiyo ndipo walikamatwa watuhumiwa wawili Joseph Kigulu(24)
mkazi wa Airport na Juma Nelson(31) mkazi wa Iyela wote jijini Mbeya na
walipohojiwa wakasema pikipiki hiyo ipo nyumbani kwa Emmanuel.
Kamanda Msangi amesema mara baada ya kwenda nyumbani
kwa kijana huyo na kufanya upekuzi ndipo alipokutwa na bunduki aina ya Shortgun
na risasi saba alizokuwa amezificha chini ya Godoro.
Amesema watuhumiwa wote wanashikiliwa na jeshi hilo
na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

No comments:
Post a Comment