Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, August 14, 2024

DC RUNGWE ATAKA MADIWANI KUKEMEA UKATILI DHIDI YA ALBINO, WATOTO


Na Mwandishi Wetu, Rungwe

MADIWANI katika Halimashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vya mauaji dhidi ya watu wenye ualbino pamoja na ukatili dhidi ya watoto.

 

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu alisisitiza hilo alipotoa salamu za serikali kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/24.

 

Haniu alisema katika maeneo mbalimbali nchini kumeanza kuonekana matukio ya mauaji dhidi ya watu walio na ualbino matukio aliyosema yamekuwa yakiibuka nyakati za kuelekea chaguzi hatua aliyosema ni imani zisizopaswa kupewa nafasi kwakuwa hakuna uhusiano kati ya uchaguzi na ualbino.