Na Mwandishi Wetu, Rungwe
MADIWANI katika Halimashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya
wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vya mauaji dhidi ya watu
wenye ualbino pamoja na ukatili dhidi ya watoto.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu alisisitiza hilo alipotoa
salamu za serikali kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili
taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa robo ya nne ya
mwaka wa fedha 2023/24.
Haniu alisema katika maeneo mbalimbali nchini kumeanza kuonekana
matukio ya mauaji dhidi ya watu walio na ualbino matukio aliyosema yamekuwa
yakiibuka nyakati za kuelekea chaguzi hatua aliyosema ni imani zisizopaswa
kupewa nafasi kwakuwa hakuna uhusiano kati ya uchaguzi na ualbino.
No comments:
Post a Comment