Uongozi wa blogu hii unaungana na watanzania wote hususani wakazi wa mkoa wa Mbeya ulio jirani na nchi ya Zambia kuitakia kila la kheri timu ya taifa ya nchi hiyo CHIPOLOPOLO katika mchezo wake na Ivory Coast unaochezwa usiku huu nchini Gabon ikiwa ni mchezo wa fainali wa michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2012
Kama ilivyo kwa wazambia pia sisi tunaamini ushindi katika mchezo wa leo ndicho kitu kitakacho saidia kutufuta majonzi yaliyotukumba mwaka 1993 baada ya wachezaji wa timu hiyo kufa nchini Gaboni kwa ajali ya ndege
Mungu ibariki timu ya taifa ya Zambia-Amina



No comments:
Post a Comment