Monday, March 3, 2014
WATATU WAKAMATWA NA NOTI BANDIA
KAMANDA wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi amewataja waliokamatwa kuwa ni Alex Fungai(25),Timoth Mgina(27) na Lusekelo Stephano(20) wote wakazi wa jijini Mbeya aliosema wanashikiliwa kwa kosa la kukutwa na noti bandia.
Amesema watuhumiwa wamekamatwa jana(Machi 2) saa 12 za jioni katika kijiji cha Ibala kata na tarafa ya Rujewa wilayani Mbarali.
Amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na noti 13 za shilingi 10,000 kila moja hivyo jumla zilikuwa na thamani ya shilingi 130,000.
Amesema kati ya fedha hizo bandia,noti saba zilikuwaa na namba BX 8365292 kila moja,mbili zilikuwa na namba BX 83 652 94 kila moja,nyingine mbili zilikuwa na namba BL 6882315 na nyingine mbili zilikuwa na namba BX 5764841. Kila moja.
Kamanda Msangi alisema watuhumiwa wa matukio yote mawili watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao bala baada ya polisi kuwafikisha kizimbani baada ya taratibu mbalimbali za kisheria kukamilishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment