Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, May 30, 2024

TULIA ADHAMINI TULIA CUP UYOLE 2024 AMWAGA 11M NA VIFAA VYA MICHEZO


Mchezaji wa zamani wa soka Simon Sanga aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa akizungumza jambo
Meneja wa Taasisi isiyo ya serikali ya Tulia Trust, Jacqueline Boaz akisalimiana na wachezaji kabla ya mtanange wa ufunguzi kuanza




Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya Sadiki Jumbe akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi


 Na Mwandishi Wetu

Michuano ya soka Tulia Trust kwa ushirikiano na Raphael Group imezinduliwa rasmi katika Uwanja wa Mawinji Uyole ya Kati Mgeni rasmi akiwa ni Simon Sanga mchezaji wa zamani wa soka.


Meneja wa Taasisi isiyo ya serikali ya Tulia Trust Jacqueline Boaz amesema michuano hiyo inadhaminiwa kwa mwaka wa nne mfululizo na taasisi hiyo ambapo mwaka huu udhamini ni wa Shilingi 11,450,000.

Boaz amesema lengo la Taasisi ni kukuza michezo na kutoa fursa ya ajira kwa vijana na jumla ya timu thelathini na nne zinashiriki michuano hiyo na kila timu imepatiwa seti ya jezi na mipira.

Awali Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa Miguu Jiji la Mbeya John Gondwe amesema michuano hiyo imekuwa ikiibua vipaji kwa vijana Jijini Mbeya.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya Sadiki Jumbe amemuomba Mgeni rasmi kuwa mdhamini wa Chama Cha Wanawake mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya.

Akijibu ombi la ulezi wa Chama Cha mpira wa Miguu Simon Sanga amekubali kuwa mlezi wa Chama hicho.

Sanga ameomba wadau kutovamia Viwanja vya michezo ili vijana wapate maeneo ya kucheza waweze kuepukana na vitendo viovu.

Hata hivyo ameomba kutilia mkazo zaidi soka la Wanawake ambalo halijapewa kipau mbele Mkoani Mbeya.

Katika kutia hamasa michuano hiyo Taasisi ya Tulia Trust itatoa zawadi kwa mfungaji bora, golikipa bora na timu yenye nidhamu.

Mshindi wa kwanza atapata kikombe na pesa shilingi milioni tano,mshindi wa pili shilingi milioni tatu,wa tatu shilingi milioni mbili na mshindi wa nne atapata shilingi milioni moja.

Golikipa bora atapata shilingi laki moja, mfungaji bora shilingi laki moja,timu yenye nidhamu itapata shilingi laki moja mfungaji na kikundi chenye hamasa kitajinyakulia pia shilingi laki moja na mwandishi bora wa michezo atajinyakulia shilingi elfu hamsini.

Wednesday, May 15, 2024

MWANA FA ALIVYONOGESHA MBEYA TULIA MARATHON 2024


 Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma(MWANA FA) akitumbuiza kwenye mashindano ya mbio ya Mbeya Tulia Marathon 2024 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust na kufanyika jijini Mbeya.

Saturday, May 11, 2024

WAZIRI MKUU AFUNGA RASMI MBEYA TULIA MARATHON 2024

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufunga rasmi mashindano ya mbio ya Mbeya Tulia Marathon 2024 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust na kufanyika jijini Mbeya.



Spika wa Bunge na Mkurugenzi wa Tulia Trust, Dk Tulia Ackson akizungumza kwenye kilele cha mashindano ya mbio ya Mbeya Tulia Marathon 2024 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust na kufanyika jijini Mbeya.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma akitumbuiza kwenye mashindano ya mbio ya Mbeya Tulia Marathon 2024 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust na kufanyika jijini Mbeya.


Msanii Bahati Bukuku akitumbuiza kwenye kilele cha mashindano ya mbio ya Mbeya Tulia Marathon 2024 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust na kufanyika jijini Mbeya.








Tuesday, May 7, 2024

WANAHABARI MBEYA KABLA YA KUKUBALI KWA MBINDE KICHAPO CHA 3-0 TOKA TULIA TRUST


 

NYOTA WA TAIFA STARS WATAKAOKWENDA SAUDI ARABIA KWA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI

 Hiki hapa kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars) kitakachokwenda Saudi Arabia kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Sudan.

Kikosi hicho kitaanza safari kesho Mei 8, 2024.

WAANDISHI MBEYA WAKUBALI KICHAPO CHA GOLI 3-0 TOKA TULIA TRUST

 

Kikosi cha Timu ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya

Kikosi cha Timu ya Tulia Trust


Kocha Amos Chuma akitoa maelekezo kwa wachechezaji wa kikosi cha Timu ya Waandishi wakati wa mapumziko.




Baadhi ya waandishi wa habari wakimpongeza mlindamlango Daniel Simelta kwa kuonesha umahiri wa kupangua michomo iliyoelekea langoni kwake kutoka Tulia Trust na kuwezesha kupunguza idadi ya magoli ya kufungwa.


 Na Mwandishi Wetu


TIMU ya soka ya waaandishi wa habari Mkoa wa Mbeya jana imechezia kichapo cha goli 3-0 kutoka kwa Timu ya Taasisi ya Tulia Trust katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye dimba la Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa.

 

Mchezo huo wa uchangamshi ulikuwa sehemu ya maandalizi ya kuelekea mashindano ya mbio ya Mbeya Tulia Marathon yanayotarajiwa kufanyika Mei 10 hadi 11 mwaka huu jijini Mbeya.

 

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Tulia Trust kuongoza kwa goli moja huku timu ya waandishi ikionesha uhai tofauti na ilivyoonekana kipindi cha pili ambapo makoya yaliyofanyika yakalifanya jahazi kuzidi kuzama kwa kuongezwa goli mbili nyingine na kufanya matokeo ya 3-0 hadi dakika 90 zinakamilika.

 

Pamoja na kipigo hicho cha goli tatu, mlinda mlango wa timu ya waandishi wa habari Daniel Simelta ndiye aliyeibuka shujaa wa mchezo huo kwani licha ya kuruhusu mabao matatu bado aliweza kuisaidia kwa sehemu kubwa timu yake kwa kuokoa mipira mingi iliyolenga golini kwake kutoka kwa washambuliaji wa Tulia Trust walioonekana kuwa na uchu wa mabao.

 

Chini ya Kocha mkongwe Amos Chuma timu ya waandishi ilionesha inahitaji muda wa kutosha kujiimarisha iwapo inahitaji kuendelea kutoa ushindani kwenye michuano mbalimbali ya mkoani humo.