Kikosi cha Timu ya
waandishi wa habari mkoa wa Mbeya
Kikosi cha Timu ya
Tulia Trust
Kocha Amos Chuma akitoa
maelekezo kwa wachechezaji wa kikosi cha Timu ya Waandishi wakati wa mapumziko.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimpongeza mlindamlango Daniel Simelta kwa kuonesha umahiri wa kupangua michomo iliyoelekea langoni kwake kutoka Tulia Trust na kuwezesha kupunguza idadi ya magoli ya kufungwa.
TIMU ya soka ya waaandishi
wa habari Mkoa wa Mbeya jana imechezia kichapo cha goli 3-0 kutoka kwa Timu ya
Taasisi ya Tulia Trust katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye dimba la
Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa.
Mchezo huo wa
uchangamshi ulikuwa sehemu ya maandalizi ya kuelekea mashindano ya mbio ya Mbeya
Tulia Marathon yanayotarajiwa kufanyika Mei 10 hadi 11 mwaka huu jijini Mbeya.
Kipindi cha kwanza
kilimalizika kwa Tulia Trust kuongoza kwa goli moja huku timu ya waandishi
ikionesha uhai tofauti na ilivyoonekana kipindi cha pili ambapo makoya
yaliyofanyika yakalifanya jahazi kuzidi kuzama kwa kuongezwa goli mbili
nyingine na kufanya matokeo ya 3-0 hadi dakika 90 zinakamilika.
Pamoja na kipigo hicho
cha goli tatu, mlinda mlango wa timu ya waandishi wa habari Daniel Simelta
ndiye aliyeibuka shujaa wa mchezo huo kwani licha ya kuruhusu mabao matatu bado
aliweza kuisaidia kwa sehemu kubwa timu yake kwa kuokoa mipira mingi iliyolenga
golini kwake kutoka kwa washambuliaji wa Tulia Trust walioonekana kuwa na uchu
wa mabao.
Chini ya Kocha mkongwe
Amos Chuma timu ya waandishi ilionesha inahitaji muda wa kutosha kujiimarisha
iwapo inahitaji kuendelea kutoa ushindani kwenye michuano mbalimbali ya mkoani
humo.
No comments:
Post a Comment