KIKUNDI cha ngoma cha Kasanga maarufu kama Ing’oma cha wilayani Rungwe kimeibuka mshindi katika mashindano ya ngoma za asili yaliyoandaliwa na kampuni ya bia ya TBL kupitia kiwanda chake cha Mbeya.
Mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha uhasibu(TIA) jijini Mbeya yalishirikisha vikundi 26 vya Ngoma kutoka wilaya za Mbeya,Rungwe,Kyela,Mbozi,Njombe na Iringa.
Kwa ushindi huo kikundi cha Kasanga kilijinyakulia kitisha cha fedha taslimu shilingi milioni moja na kikombe.
Nafasi ya msindi wa pili ilikwenda kwa kikundi cha Lipango kutoka kata ya Isansa wilayani Mbozi ambacho kilizawadiwa fedha taslimu shilingi laki tano.
Nafasi ya tatu ilikwenda kwa kikundi cha Mbeta kutoka Isyesye jijini Mbeya ambacho kilizawadiwa shilingi laki mbili wakati vikundi vingine shiriki vilipewa kifuta jasho cha shilingi 50,000 kila kimoja.
Mkuu wa matukio wa kampuni ya TBL kanda ya Mbeya, Geophray Mwangungulu alisema lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha wananchi kupenda ngoma za asili pamoja na utamaduni wao.
Mwangungulu alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watanzania kusahau asili zao kutokana na ujio wa sayansi na teknolojia hatua inayohitaji wadau kufikiri namna nzuri ya kuwezesha utamaduni wa makabila ya kiafrika kudumishwa.
Alitaja nyimbo na ngoma za asili kuwa miongoni mwa mambo muhimu yanayoweza kuiwezesha jamii ya kiafrika kuzikumbuka na kudumisha mila zao katika kipindi hiki ambacho tamaduni za kimagharibi zinaonekana kuenea kwa kasi katika mataifa mengi duniani.
Friday, September 27, 2013
KASANGA WANYAKUA MILIONI MOJA YA MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI

Wednesday, September 25, 2013
7 WAJISHINDIA PIKIPIKI ZA AMSHA MAISHA YAKO NA COCA COLA
Saturday, September 21, 2013
T.PRISONS YATOSHANA NGUVU NA MTIBWA SUGAR.SHABIKI WAJIKUTA WAKO SOKOINE MBEYA WANASHANGILIA MECHI YA DAR ES SALAAM KATI YA MBEYA CITY NA SIMBA SC
Saturday, September 14, 2013
DIWANI WA CHADEMA MBARONI AKITUHUMIWA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI
Friday, September 13, 2013
HOMA YA MCHEZO KATI YA MBEYA CITY NA YANGA YAZIDI KUPANDA.MULUGO AAHIDI MILIONI MBILI MBEYA CITY IKISHINDA
Wednesday, September 11, 2013
MAITI YA KICHANGA YAOKOTWA KWENYE KITUO CHA MAFUTA
MAITI ya mtoto mchanga mwenye umri wa siku moja imeokotwa ikiwa imetelekezwa katika mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe.
Maiti ya mtoto huyo mwenye jinsi ya kike imeokotwa jana(Septemba 10) mwaka huu majira ya saa nane mchana katika mtaa wa Bagamoyo nyuma ya kituo cha mafuta cha Caltex kilichopo mtaani hapo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman amesema leo kuwa mwili huo ulikuwa umeviringishwa kipande cha kitenge na kisha kuwekwa kwenye mfuko wa plastic maarufu kama Rambo.
Kamanda Athuman amesema juu ya mfuko huo liliwekwa jiwe hali iliyodhihirisha mama wa mtoto huyo ambaye hajafahamika alimuua mwanaye baada ya kujifungua.
Amesema jeshi la polisi linaendelea na msako ili mama wa mtoto huyo aweze kuchukuliwa hatua stahiki kutokana na tukio la kinyama alilotenda.
Tuesday, September 3, 2013
WAPENDEKEZA KUBORESHWA KWA BAADHI YA IBARA ZILIZOPO KWENYE RASIMU YA KATIBA MPYA YA TANZANIA

WAKAZI wialayni Sumbawanga mkoani Rukwa wamependekeza kufanyiwa marekebisho kwa ibara ya 72,ibara ndogo ya 5 na 6 sehemu ya A na B ya rasimu ya katiba mpya ambapo tume imependekea rais anapofariki nafasi yake ichukuliwe na mgombea aliyeshika nafasi ya pili kwa wingi wa kura katika matokeo ya uchaguzi uliomweka madarakani.
Wakichangia maoni yao kwenye mdahalo wa kupitia na kujadili rasimu hiyo ulioandaliwa na asasi ya vikundi vya wakulima wadogo wilayani Humo(Umawawa) uliofanyika katika kata ya Kaengesa baadhi ya washiriki wamesema kuwa uwepo wa ibara hiyo unaweza kusababisha mshindi wa pili kwenye uchaguzi husika kufanya njama za kumuua rais kwa tamaa ya kushika madaraka baada ya kifo.
Mmoja wa wachangia hoja hiyo Fulgency Songoro amesema amependekeza katiba kutoa fursa ya kufanyika kwa uchaguzi mpya iwapo itatokea rais aliyepo madarakani amefariki dunia akisema hiyo italeta usawa wa kidemokrasia kwa wananchi kutumia masanduku ya kura kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Songoro pia amependekeza,pamoja na kubaki ikulu wakati wa kampeni za uchaguzi,katiba pia isimpe fursa rasi ya kutoa tamko lolote linalohusiana na uchaguzi badala yake aendelee na majukumu yake kama kawaida.
Monday, September 2, 2013
MTOTO AGONGESHWA UKUTANI AFARIKI DUNIA
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Mbeya akiwemo la mtoto kugongeshwa ukutani.
Kifo cha mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Aines Zacharia mwenye umri wa miezi mine mkazi wa kijiji cha Ivuna wilayani Momba kilitokea Septemba mosi saa saba mchana alipokuwa akiendelea kupata matibabu katika kituo cha afya Kamsamba wilaya hapo.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Barakael Masaki alisema awali kulikuwa na ugomvi kati ya mama wa mtoto huyo aliyemtaja kwa jina la Priscar Willson aliyekuwa amembeba mgongoni na mumewe Steven Cletus.
Alisema kufuatia ugomvi huo Cletus alimsukuma mwanamke huyo na ndipo wakajikuta wanamgongesha mtoto ukutani na kumsababishia jeraha kubwa kichwani na ndipo mtuhumiwa alipokimbilia kusikojulikana na anatafutwa.
Katika tukio jingine mtu aliyefahamika kwa jina moja la Oscar anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30 na 35 amefariki dunia baada ya kudondoka kutoka katika gari.
Masaki alisema ajali hiyo ilitokea Septemba mosi saa 4:45 asubuhi maeneo ya Mabatini jijini Mbeya katika barabara ya Meta/stendi kuu na kutaja gari husika kuwa ni namba T 773 BNL iliyokuwa ikiendeshwa na Deston Kabissa(29) mkazi wa Sae jijini hapa.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya na kuwa dereva anaendelea kushikiliwa wakati uchunguzi zaidi juu ya ajali hiyo ukiwa unaendelea.
Subscribe to:
Comments (Atom)