Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya
Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile amesisitiza kuwa michezo ni muhimu katika
kuimarisha Afya na Uchumi wa wananchi hivyo ni muhimu kila mwanajamii wakiwemo
watumishi kuizingatia.
Chirukile ameyasema
hayo wakati akifungua Bonanza la Michezo la watumishi lililofanyika katika Uwanja
wa Kumbukumbu wa Nelson Mandela uliopo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani
Rukwa.
Chirukile amesema kuwa
michezo sio tu hufungua fursa za kiuchumi, bali pia huimarisha undugu na
mshikamano baina ya jamii.
"Michezo ni afya,
michezo hufungua fursa za uchumi na kuimarisha undugu baina ya Jamii hivyo
mabonanza kama haya yafanyike mara kwa mara ili kuchechemua maendeleo endelevu
baina yetu," amesema Chirukile.
Aidha Mkuu huyo wa
Wilaya amesisitiza kuwa Serikali inaunga mkono michezo katika jamii na
kuwahamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za michezo ili kuboresha afya
zao na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Bonanza hilo
limehusisha timu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Wilaya ya Mbozi
na Wilaya ya Nkasi, zikishindana katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa
miguu, mpira wa pete, mpira wa mikono, mpira wa wavu, bao, drafti, na karata.



No comments:
Post a Comment