Na Joachim Nyambo,Mbeya
RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) ambaye pia ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Uyole Dkt Tulia Ackson amekabidhi nyumba ya 25 kwa Elizabeth Jimmy (72) mkazi wa Mtaa wa Mwasote Kata ya Itezi Jijini Mbeya.
Kabla ya kukabidhi nyumba Dkt Tulia Ackson amepokea bendera ya upendo kutoka kwa kiongozi wa mbio za bendera Lugano Mwangosi ambapo kaya 160 zenye watu zaidi ya watu 1000 zilinufaika kupitia mbio hizo kwa kupewa chakula.
Mwangosi amesema katika mbio hizo pia wamebaini changamoto mbalimbali zinazoikabili wahitaji wakiwemo watu wenye ulemavu wanaohitaji Viti mwendo na miguuni bandia.
Diwani wa Kata ya Itezi, James Kapolesya amekabidhi kitanda na godoro kwa nia ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mbunge.
Katika hotuba yako Dkt Tulia Ackson amesema Taasisi ya Tulia Trust amesema Taasisi yake hujenga nyumba kutokana na uhitaji kama kuna mtu anaona nyumba ni ndogo na atatamani kuishi hapo alete hitaji lake ili vyumba viongezwe.
Dk Tulia Ackson amesema wahitaji ni wengi hivyo tupendane katika jamii kwa kusaidia watu wenye uhitaji hata kwa kuwasaidia chakula.
Amesema hoja za wakimbiza bendera amezipokea wakiwemo wa matibabu na watu wenye ulemavu wanaohitaji Viti mwendo watapatiwa baada ya sikukuu.
Amesema mpango wa mwaka huu ni kujenga nyumba moja kila Kata hivyo zitajengwa nyumba 13 na ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote waliomuunga mkono kwa kutoa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula, nguo na mablanket.
Amehitimisha kuwa shughuli za kuisadia jamii ni endelevu zikiwemo kusomesha, matibabu na ujenzi wa nyumba.
Spika mstaafu wa Uswisi Maya Riniker kupitia Chama cha FDP amempongeza Dkt Tulia Ackson kwa namna anavyoisaidia jamii kwa kutoa misaada mbalimbali na amefurahi kwa namna wananchi wanavyozikubali kazi zake.
Chifu George Lyoto kwa niaba ya Viongozi wa mila amepongeza juhudi zinazofanywa na Mbunge pia amesema wapuuzwe wanaobeza kazi zinazofanywa na Mbunge.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Kata ya Itezi Jijini Mbeya, Raphael Mwaitege amelaani vikali la watu wanaobeza zoezi la ujenzi wa nyumba za wahitaji linalofanywa na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Uyole Dkt Tulia Ackson kuwa nyumba zinazojengwa kuwa ni ndogo wakati wao hawajawahi kutoa hata misumari.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Itezi Gervas Lameck Lonje amesema njia pekee ya kushikamana na Dkt Tulia Ackson ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa za kuwasaidia wahitaji.
Aidha Mwenyekiti wa
Jumuya ya Wazazi Wilaya ya Mbeya Mjini, Emmanuel Mwalupindi ambaye
alimwakilisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mbeya Mjini amesema kwa
sasa hakuna muda wa kusikiliza maneno bali ni wakati wa kufanya kazi kwa
vitendo kwani kila mmoja akisaidia wahitaji atakuwa anapata thawabu mbele za
Mungu.
Kwa upande wake
Elizabeth Jimmy amemshukuru sana Dk Tulia Ackson kwa kumjengea nyumba ya kudumu
kwani imemuondokea kadhia ya kupanga iliyokuwa inamkabili.