Wednesday, November 20, 2024
Saturday, November 16, 2024
TYSON AAMBULIA KICHAPO
Jake Paul amemshinda bondia nguli Mike Tyson kupitia uamuzi wa Pamoja katika mpambano wa uzito wa juu uliofanyika Texas Marekani. Pigano kati ya Paul, mtengeneza maudhui mwenye umri wa miaka 27 na Tyson, bingwa wa zamani wa uzito wa juu mwenye umri wa miaka 58, halikuwaridhisha mashabiki.
Mkongwe Tyson hakuweza kuonesha makali dhidi ya mpinzani wake huyo chipukizi. Tyson alimrushia ngumi 18 tu wakati Paul akimnyeshea nvua ya ngumi 78. Pigano hilo lilienda raundi zote nane. Jaji mmoja alimpa Paul pointi 80 dhidi ya 72 wakati wengine wawili wakimpa pointi 79-73.
"Kwanza kabisa, Mike Tyson – ni heshima kupambana naye ulingoni," alisema Paul. Mike, yeye ni mkongwe, nimetiwa moyo naye, na tusingekuwa hapa leo bila yeye.”
Naye Tyson baada ya kichapo alisema, “Nilijua ni bondia mzuri. Alikuwa amejiandaa. Nilikuja kupigana. Sikumdhihirishia yeyote kitu, ila mimi mwenyewe.”
Kwa hisani ya DW
Friday, November 15, 2024
KAMANDA KUZAGA ATOA SOMO KWA WANAVYUO MBEYA AKIFUNGUA DREAMS INTERCOLLEGE
Na Mwandishi Wetu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amewataka wanavyuo mkoani Mbeya kujiepusha na vitendo visivyofaa katika jamii ikiwemo uhalifu.
Hayo ameyasema Novemba 14, 2024 wakati akifungua mashindano ya mpira wa miguu yanayohusisha vyuo vikuu mkoani humo yanayojulikana kama "Dreams Intercollege" yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya.
Aliongeza kuwa, mashindano hayo yakawe chachu katika kuibua vipaji vya mpira wa miguu kwa wanavyuo mkoani humo kwani michezo ni ajira hivyo alisisitiza kutumia vizuri fursa ya kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Naye, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mbeya Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Veronica Ponera amewataka wanavyuo mkoani humo kujiepusha na ukatili wa kijinsia, kujiepusha na tamaa ya vitu vya thamani ambavyo vinaweza kuwaingiza kwenye vishawishi vya vitendo viovu.
"Jeshi la Polisi nchini linaendelea na kampeni ya Tuwaambie kabla hawajaharibiwa hivyo ni nafasi kwetu kuwaeleza wanavyuo mambo ya kujiepusha nayo kabla hamjaharibikiwa na kupoteza dira ya kufikia ndoto zenu" alisema ASP Ponera.
Awali akizungumza Mratibu wa mashindano hayo Meneja wa kituo cha redio"Dreams fm" cha Jijini Mbeya ndugu Samuel Mhina amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha wanavyuo wote waliopo mkoani Mbeya, T.I.A ambaye ni bingwa mtetezi, CUoM, Tumaini, MUST, Chuo cha Afya - Ifisi yakiwa na lengo la kujenga umoja na kuibua vipaji.
Mechi ya ufunguzi ambayo iliwakutanisha chuo kikuu cha katoliki Mbeya (CUoM) dhidi ya T.I.A imemalizika kwa kushuhudia CUoM ikiibuka na ushindi wa magoli matano kwa bila na kukabidhiwa ngao ya jamii ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mashindano hayo.
YANGA YAACHANA RASMI NA GAMOND
Uongozi wa klabu ya Yanga Sc umethibitisha kuvunja mkataba na kocha wa kikosi cha kwanza Miguel Angel Gamondi raia wa Argentina pamoja na kocha msaidizi Moussa Ndaw.
Taarifa ya leo Novemba 15, 2024 iliyotolewa na klabu hiyo imebainisha kuwa klabu hiyo tayari imeanza mchakato wa haraka wa kutafuta Makocha wapya wa kikosi hicho na unatarajiwa kukamilika hivi punde.
Thursday, November 14, 2024
KING KIKII AFARIKI DUNIA
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Boniface Kikumbi maarufu King Kikii amefariki dunia.
Mwanamuziki huyo ambaye ameugua kwa muda mrefu, amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 15 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu
Marehemu King Kikii atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Kwa miaka mingi ameburudisha, amefundisha na kuelimisha jamii kupitia nyimbo zake.
Enzi za uhai wake,Marehemu King Kikiii alitamba na vibao mbalimbali kikiwemo cha 'Kitambaa cheupe'.
King Kikii alikuwa Mtunzi na mwimbaji wa zamani wa Marquiz du Zaire na Orchestra Double O ambaye pia alikuwa mmiliki wa bendi ya La Capital, inayotesa na mtindo wake wa Kitambaa Cheupe
Alizaliwa mwaka 1947 katika Jiji la Lubumbashi lililopo kwenye Mkoa wa Katanga, eneo maarufu huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC)
Sunday, November 3, 2024
Subscribe to:
Comments (Atom)









