Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Boniface Kikumbi maarufu King Kikii amefariki dunia.
Mwanamuziki huyo ambaye ameugua kwa muda mrefu, amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 15 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu
Marehemu King Kikii atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Kwa miaka mingi ameburudisha, amefundisha na kuelimisha jamii kupitia nyimbo zake.
Enzi za uhai wake,Marehemu King Kikiii alitamba na vibao mbalimbali kikiwemo cha 'Kitambaa cheupe'.
King Kikii alikuwa Mtunzi na mwimbaji wa zamani wa Marquiz du Zaire na Orchestra Double O ambaye pia alikuwa mmiliki wa bendi ya La Capital, inayotesa na mtindo wake wa Kitambaa Cheupe
Alizaliwa mwaka 1947 katika Jiji la Lubumbashi lililopo kwenye Mkoa wa Katanga, eneo maarufu huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC)

No comments:
Post a Comment