Mwakilishi wa Kampuni ya Achimwene Safaris,Emmanuel Mwalupindi akipokea cheti cha utambuzi wa mchango wa kampuni hiyo katika mashindano ya mwaka huu kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust,Dk Tulia Ackson
KAMPUNI ya Achimwenye
Safaris imeahidi kuendelea kuyaunga mkono Mashindano ya Mbio ya Tulia Marathon
ikisema inavutiwa na umuhimu wake ndani ya jamii hususani kwa kutumia kukusanya
fedha kwaajili ya kuimarisha huduma za kijamii.
Miongoni mwa mambo yanayotajwa
kuivutia Kampuni ya Achimwene Safari ni pamoja na fedha zinazokusanywa kupitia
Tulia Marathon kutumika kuimarisha miundombinu hususani majengo ya sekta za
Elimu na Afya na pia kuboresha maisha ya kaya zenye uhitaji.
Mwakilishi wa kampuni
hiyo, Emmanuel Mwalupindi amebainisha hayo alipotoa salamu za kampuni kwenye kilele
cha Mashindano ya Mbio za Betika Mbeya Tulia Marathon 2026 yaliyofanyika jijini
Mbeya ikiwa ni msimu wa 10 huku Achimwene Safari ikiwa ni miongoni mwa wadau
waliofadhili.
“Tunaridhishwa kwa
namna mashindano yanavyofanyika,ni faraja kuona fedha zinazokusanywa zinakwenda
kuisaidia jamii iliyo na uhitaji.Sisi Achimwene Safari tunakuahid Mkurugenzi
kuwa tutazidi kuwa nawe bega kwa bega..hatutokuacha.” amesema Mwalupindi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust iliyoandaa mashindano hayo,Dk Tulia Ackson
ameipongeza kampuni ya Achimwene Safaris kwa kuunga mkono juhudi za taasisi
hiyo kwa kuwa sehemu ya wadhamini ili kufikia adhma ya kuwafikia wenye uhitaji.
Dk Tulia ambaye pia ni
Mbunge wa Uyole,Spika wa Bunge mstaafu na Rais wa Mabunge Duniani(IPU) amewataka
wadau wengine wakiwemo wa usafiri kuiga mfano wa Achimwene Safaris kushiriki
kwa kufadhili mashindano hayo kwakuwa pamoja na faida nyingine pia yanafunguwa
fursa katika nyanja ya usafirishaji kutokana na wageni wanaofika mkoani Mbeya
kushiriki.
Mashindano ya Betika
Mbeya Tulia Marathon mwaka huu pia
yamehudhuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo,Gerson Msigwa aliyemwakilisha Waziri wa Wizara hiyo,Paul Makonda huku
pia wasanii mbalimbali maarufu wa tasnia
ya uigizaji na wao wakishiriki mbio hizo.
No comments:
Post a Comment