Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, May 22, 2026

MADIWANI MBARALI WALIVYOTEMBELEA MRADI WA UJENZI WA UWANJA WA KISASA ARUSHA








Na Mwandishi Wetu

Ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kujifunza na kupata uzoefu kwenye masuala mbalimbali Jijini Arusha kati ya Mei 14 - 18, 2026, Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakiwa wameambatana na Timu ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, wametembelea na kujionea uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu unaojengwa Jijini humo.


Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ambaye ameongoza ujumbe huo, Charles Komba ameipongeza Serikali kwa uwekezaji huo ambao unaonesha dhamira ya dhati katika kuinua sifa ya nchi ya Tanzania kupitia sekta ya michezo ambapo kukamilika kwa uwanja huo ni uthibitisho kwa nchi yetu kuwa tayari kwa michuano ya AFCON 2027 na michuano mingine yenye hadhi kitaifa na kimataifa.


“Wanambarali tunampongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha michezo kwa vitendo, uwanja huu ni uthibitisho kuwa Tanzania tuko tayari kwa AFCON 2027, na sisi Mbarali tunamuunga mkono kwa kuwa tumetambua fursa za uwekezaji kupitia mradi huu na tuko tayari kuzitumia”, amesema Komba.

No comments:

Post a Comment