Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, May 14, 2026

MWASITI NA BARBARA WAKABIDHI TAULO ZA KIKE SHULE YA SEKONDARI IDUDA












Na Mwandishi Wetu

KUELEKEA mbio za Betika Mbeya Tulia Marathon 2026 Mabalozi wa Tulia Trust, Mwasiti Almas Yusuph maarufu kama Mwasiti na Barbara Hassan wamefika katika shule ya sekondari Iduda iliyopo katika Kata ya Iduda Jimbo la Uyole Jijini Mbeya.

 

Mabalozi hawa wamefika shuleni hapo kwa lengo kuu la kufanya mdahalo na wanafunzi wa shule wenye mada isemayo “Maisha kabla ya umaarufu na safari ya mafanikio” huku pia wakigawa taulo za kike.

 

Mdahalo huu umefanyika kupitia simulizi za wageni maarufu ambapo ikiaminiwa kuwa wanafunzi watajifunza kuwa mafanikio hayaji kwa bahati, bali hujengwa kwa nidhamu, kujituma na kutokukata tamaa.


No comments:

Post a Comment