Saturday, May 30, 2026
Friday, May 22, 2026
MADIWANI MBARALI WALIVYOTEMBELEA MRADI WA UJENZI WA UWANJA WA KISASA ARUSHA
Na Mwandishi Wetu
Ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kujifunza na kupata uzoefu kwenye masuala mbalimbali Jijini Arusha kati ya Mei 14 - 18, 2026, Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakiwa wameambatana na Timu ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, wametembelea na kujionea uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu unaojengwa Jijini humo.
Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ambaye ameongoza ujumbe huo, Charles Komba ameipongeza Serikali kwa uwekezaji huo ambao unaonesha dhamira ya dhati katika kuinua sifa ya nchi ya Tanzania kupitia sekta ya michezo ambapo kukamilika kwa uwanja huo ni uthibitisho kwa nchi yetu kuwa tayari kwa michuano ya AFCON 2027 na michuano mingine yenye hadhi kitaifa na kimataifa.
Thursday, May 21, 2026
Saturday, May 16, 2026
ACHIMWENE SAFARI YAAHIDI MAKUBWA TULIA TRUST MARATHON
Mwakilishi wa Kampuni ya Achimwene Safaris,Emmanuel Mwalupindi akipokea cheti cha utambuzi wa mchango wa kampuni hiyo katika mashindano ya mwaka huu kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust,Dk Tulia Ackson
KAMPUNI ya Achimwenye
Safaris imeahidi kuendelea kuyaunga mkono Mashindano ya Mbio ya Tulia Marathon
ikisema inavutiwa na umuhimu wake ndani ya jamii hususani kwa kutumia kukusanya
fedha kwaajili ya kuimarisha huduma za kijamii.
Miongoni mwa mambo yanayotajwa
kuivutia Kampuni ya Achimwene Safari ni pamoja na fedha zinazokusanywa kupitia
Tulia Marathon kutumika kuimarisha miundombinu hususani majengo ya sekta za
Elimu na Afya na pia kuboresha maisha ya kaya zenye uhitaji.
Mwakilishi wa kampuni
hiyo, Emmanuel Mwalupindi amebainisha hayo alipotoa salamu za kampuni kwenye kilele
cha Mashindano ya Mbio za Betika Mbeya Tulia Marathon 2026 yaliyofanyika jijini
Mbeya ikiwa ni msimu wa 10 huku Achimwene Safari ikiwa ni miongoni mwa wadau
waliofadhili.
“Tunaridhishwa kwa
namna mashindano yanavyofanyika,ni faraja kuona fedha zinazokusanywa zinakwenda
kuisaidia jamii iliyo na uhitaji.Sisi Achimwene Safari tunakuahid Mkurugenzi
kuwa tutazidi kuwa nawe bega kwa bega..hatutokuacha.” amesema Mwalupindi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust iliyoandaa mashindano hayo,Dk Tulia Ackson
ameipongeza kampuni ya Achimwene Safaris kwa kuunga mkono juhudi za taasisi
hiyo kwa kuwa sehemu ya wadhamini ili kufikia adhma ya kuwafikia wenye uhitaji.
Dk Tulia ambaye pia ni
Mbunge wa Uyole,Spika wa Bunge mstaafu na Rais wa Mabunge Duniani(IPU) amewataka
wadau wengine wakiwemo wa usafiri kuiga mfano wa Achimwene Safaris kushiriki
kwa kufadhili mashindano hayo kwakuwa pamoja na faida nyingine pia yanafunguwa
fursa katika nyanja ya usafirishaji kutokana na wageni wanaofika mkoani Mbeya
kushiriki.
Mashindano ya Betika
Mbeya Tulia Marathon mwaka huu pia
yamehudhuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo,Gerson Msigwa aliyemwakilisha Waziri wa Wizara hiyo,Paul Makonda huku
pia wasanii mbalimbali maarufu wa tasnia
ya uigizaji na wao wakishiriki mbio hizo.
Friday, May 15, 2026
UWANJA WA YANGA KUMILIKIWA NA KAMPUNI
RAIS wa Klabu ya Yanga
Eng.Hers Said amesema Klabu ya Yanga itafungua kampuni itakayohusika na umiliki
wa Uwanja utakaojengwa ili kuepusha migongano ya kimaslahi baina ya wamiliki wa
timu na wa uwanja.
“Hii itakuwa ni speho
project na lazima iwe na uongozi wake,iwe na umiliki wake.Klabu inataka kujenga
uwanja na mwekezaji ameshapatikana.Hivyo klabu ya Yanga kwa kushirikiana na
mwekezaji wetu tutafungua kampuni.”
“Kampuni hiyo ndiyo
itakayomiliki uwanja na katika kampuni hiyo itakayomiliki uwanja asilimia
hamsini itakwenda kwa Young Africans na asilimia 50 itakwenda kwa mwekezaji.”
“GSM amekubali kumiliki
uwanja kwa asilimia 50/50 na Yanga. GSM hana tamaa, angekuwa na tamaa basi
angesema anataka asilimia 80. Tunajua wapo wenye tamaa na tunawajua. Ukiacha
msemo wa Yanga Bingwa, hatimaye GSM ametupatia msemo mwingine, kuanzia sasa
Msemo wetu ni “GSM HANA TAMAA” Eng. Hersi
Amesema mchango wa
Yanga kwenye mradi huo wa uwekezaji mpya ni kutoa ardhi yake inayojengwa
uwanja.
Thursday, May 14, 2026
MWASITI NA BARBARA WAKABIDHI TAULO ZA KIKE SHULE YA SEKONDARI IDUDA
Na Mwandishi Wetu
KUELEKEA mbio za Betika
Mbeya Tulia Marathon 2026 Mabalozi wa Tulia Trust, Mwasiti Almas Yusuph maarufu
kama Mwasiti na Barbara Hassan wamefika katika shule ya sekondari Iduda iliyopo
katika Kata ya Iduda Jimbo la Uyole Jijini Mbeya.
Mabalozi hawa wamefika
shuleni hapo kwa lengo kuu la kufanya mdahalo na wanafunzi wa shule wenye mada
isemayo “Maisha kabla ya umaarufu na safari ya mafanikio” huku pia wakigawa
taulo za kike.
Mdahalo huu umefanyika
kupitia simulizi za wageni maarufu ambapo ikiaminiwa kuwa wanafunzi watajifunza
kuwa mafanikio hayaji kwa bahati, bali hujengwa kwa nidhamu, kujituma na
kutokukata tamaa.































