Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, November 16, 2024

TYSON AAMBULIA KICHAPO


Jake Paul amemshinda bondia nguli Mike Tyson kupitia uamuzi wa Pamoja katika mpambano wa uzito wa juu uliofanyika Texas Marekani. Pigano kati ya Paul, mtengeneza maudhui mwenye umri wa miaka 27 na Tyson, bingwa wa zamani wa uzito wa juu mwenye umri wa miaka 58, halikuwaridhisha mashabiki.

Mkongwe Tyson hakuweza kuonesha makali dhidi ya mpinzani wake huyo chipukizi. Tyson alimrushia ngumi 18 tu wakati Paul akimnyeshea nvua ya ngumi 78. Pigano hilo lilienda raundi zote nane. Jaji mmoja alimpa Paul pointi 80 dhidi ya 72 wakati wengine wawili wakimpa pointi 79-73.

"Kwanza kabisa, Mike Tyson – ni heshima kupambana naye ulingoni," alisema Paul. Mike, yeye ni mkongwe, nimetiwa moyo naye, na tusingekuwa hapa leo bila yeye.”

Naye Tyson baada ya kichapo alisema, “Nilijua ni bondia mzuri. Alikuwa amejiandaa. Nilikuja kupigana. Sikumdhihirishia yeyote kitu, ila mimi mwenyewe.”

Kwa hisani ya DW

No comments:

Post a Comment