Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, March 29, 2013

BABA AMUUA MWANAE NA KUMZIKA SEBULENI KWAKE

MTOTO Debora Riziki(3) mkazi katika kitongoji cha Iponjola kijiji cha Isange wilayani Rungwe ameuawa na kisha kufukiwa katika shimo ndani ya nyumba ya baba yake mzazi. Baba wa mtoto Debora aliyefahamika kwa jina la Riziki Mwangoka(27) mkazi wa Iponjola ndiye aliyetajwa kuhusika na mauaji ya mwanaye yaliyogundulika Machi 27 mwaka huu majira ya saa 7:40 mchana nyumbani kwa mzazi huyo. Chanzo cha mauaji hayo kimetajwa kuwa ni mgogoro wa ndoa baina ya Mwangoka na aliyekuwa mkewe Esther Mwambenja(23) anayeishi kwa sasa katika kitongoji cha Kibumbwe kijijini Kiwira wilayani hapo. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani athumani alisema mgogoro wa wanandoa hao waliotengana katika kipindi kisichojulikana ulipelekea wawili hao kuwa na mvutano wa nani aishi ni mtoto wao Debora. Kamanda Athuman alisema kufuatia hali hiyo mnamo Novemba 28 mwaka jana majira ya saa 11:00 jioni Mwangoka alimchukua kwa nguvu mtoto Debora kutoka kwa mama yake na kuondoka nae kijijini kwao. Alisema baada ya kufika huko pasipo huruma wala uchungu na damu yake alimuua mwanaye huyo na kisha kuchimba shimo katika sebule ya nyumba yake na kisha kumzika humo na kufukia. Alifafanua kuwa pasipo hofu yoyote,baba huyo aliendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo yenye kaburi la mwanae ndani hadi juzi ilipogundulika siri aliyoificha katika kipindi hicho chote. Kamanda huyo alisema baada ya kugundulika mwili wa mtoto Debora ulifukuliwa na daktari kuufanyia uchunguzi kisha ukakabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya kuuzika. Kwa mujibu wa Diwani mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na polisi wakati taratibu mbalimbali zikiendelea ili aweze kufikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment