BAADA ya kusuasua kwa kipindi cha miaka mine iliyopita hatimaye mashindano ya mbio za baiskeli jijini Mbeya yamefanyika mwishoni mwa wiki jana.

Katika mashindano hayo ya kilometa 140 Mashaka Jonas aliibuka bingwa baada ya kutumia masaa matatu na dakika 47 akiwaacha washiriki wengine 15.

Mshindi wa pili alikuwa Kiang Samson aliyetumia masaa matatu na dakika 59 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Jailos John aliyetumia muda wa masaa manne na dakika 11 kumaliza kilometa hizo.

Mshindi wa kwanza wa mbio hizo zilizondaliwa na kampuni ya Range of Vision Marketing Limited(RVMCL) ya jijini Mbeya alizawadia jumla ya shilingi laki 1.5,mshindi wa pili shilingi 100,000 na wa tatu shilingi 50,000.
Akikabidhi zawadi hizo afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya jiji la Mbeya Vicent Msola kwa niaba ya mkuu wa mkoa Abbas Kandoro alisema mbio za baiskeli ni miongoni mwa michezo inayotambuliwa na serikali na kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau wanaoandaa mashindano hayo.
Msola alisema jamii inapaswa kutambua umuhimu wa michezo na kusisitiza kufufuliwa kwa michezo mbalimbali ambayo kwa sasa inaonekana kutochezwa ili kutoa fursa kwa vijana kushiriki kwa kila mmoja na kipaji chake.
No comments:
Post a Comment