Tuesday, March 19, 2013
MWANAFUNZI MBARONI KWA NOTI BANDIA
WATU wawili akiwemo mwanafunzi wa shule ya sekondari Ndembela wilayani Rungwe wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukamatwa na noti bandia.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman alisema watu hao walikamatwa jana (Machi 18) majira ya saa 1:20 asubuhi katika Benki ya NBC tawi la Tukuyu wilayani Rungwe.
Kamanda Athuman aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni mwanafunzi Chasco Nsaji(18) waliyekuwa na mkulima Hanberd Sanga(49) mkazi wa eneom la Kiwira road katika mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe.
Alisema kwa pamoja watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na noto bandia nane zenye thamani ya shilingi 10,000 kila moja wakiwanataka kuingiza fedha hizo kwenye akaunti ya shule kwaajili ya malipo ya karoya mwanafunzi huyo.
Alisema mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo Ezekia Mwambwanji(50) ndiye aliyebaini fedha hizo kuwa zilikuwa bandia na kuamua kutoa taarifa kituo cha polisi na kuwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wote.
Alisema kati ya noti hizo noti tatu zilikuwa na namba AA 4243040,na nyingine moja moja zilikuwa na namba AA 0012030,CQ 1547949,BH 0012032,BF 1547938 na DT 1547949.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment