Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, June 24, 2026

JELA MIAKA 20 KWA SHAMBULIO LA AIBU

 


Na Mwandishi Wetu,

MAHAKAMA ya Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya imemhukumu Almas Ramadhani Almas (35) mkazi wa Chokaa Wilayani Chunya kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la shambulio la aibu alilolitenda kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu (Jina limehifadhiwa).


Hukumu hiyo imetolewa Juni 23, 2026 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Chunya Mhe James Mhanuzi. Imeelezwa kuwa Mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 25, 2026 Kijiji cha Mlimanjiwa Wilayani Chunya baada ya kumkuta mtoto mwenye umri wa miaka mitatu akicheza na wenzake ndipo alimshika mkono na kumpeleka nyuma ya nyumba na kuanza kumshika sehemu zake za siri.

Wakati akiendelea na kitendo hicho, mtu mmoja ambaye anaishi jirani na eneo hilo alimuona Mshitakiwa kupitia dirishani akimfanyia vitendo vya aibu na uzalilishaji mtoto huyo ndipo alitoa taarifa kwa watu wengine na kufanikiwa kumkamata.

Mwendesha Mashitaka Mkuu Wilaya ya Chunya Mwajabu Tengeneza na Wakili wa Serikali Pastory Machupa waliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa Mshitakiwa ili iwe funzo kwa watu wengine wenye tabia za uzalilishaji na ukatili dhidi ya watoto ili kutokomeza vitendo hivyo katika jamii. 

No comments:

Post a Comment