Saturday, September 19, 2026
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI YASHIRIKI MAZISHI YA MTENDAJI WA KIJIJI
Monday, September 14, 2026
CARITAS YAKABIDHI VIFAA KUWANOA KIUFUNDI WANAWAKE 70 KUPITIA VETA CHUNYA
MENEJA wa Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)Kanda ya Kusini Magharibi,Chololo
Omar(kulia) akipokea vifaa kutoka kwa
Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Kiimani katika Malezi,Makuzi na
Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka Shirika la Caritas Jimbo Kuu Katoliki la
Mbeya,Deogratius Kibona.Vifaa hivyo vitatumika kufundishia wanufaika wa mradi
huo watakaopata mafunzo ya ufundi mbalimbali kupitia Chuo cha Veta wilayani
Chunya.
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Caritas
Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya limekabidhi vifaa mbalimbali vya kufundishia kwa
Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi(Veta) wilayani Chunya.
Msaada huo umetolewa
kwaajili ya kuiongezea uwezo wa ufundishaji Veta kupitia Mradi wa Kuimarisha
Mifumo ya Kiimani katika Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ambapo
wanawake 70 wanufaika wa mradi huo watapata mafunzo ya ufundi mbalimbali chuoni
hapo.
Akikabidhi vifaa
hivyo,Mratibu wa mradi huo,Deogratius Kibona amesema mradi unalenga kuwawezesha
kiuchumi wanawake hao walio na watoto wenye umri wa kati ya miaka sifuri hadi
mitatu kupitia shughuli za ujasiriamali.
Akipokea vifaa hivyo,Meneja
wa Veta Kanda ya Kusini Magharibi,Chololo Omar amewataka wanufaika wa mradi huo
na kutumia vyema muda wa mafunzo watakapokuwa chuoni hapo ili baada ya kuhitimu
wakawe mfano wa kuigwa ndani ya jamii kwa kujiingizia kipato kupitia
ujasiriamali na ufundi.






