Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imeshiriki mazishi ya aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Kapunga Kata ya Itamboleo, marehemu Zephaniah Mgaya, aliyefariki dunia tarehe 16 Septemba 2026 wakati akipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
Katika msiba huo, Halmashauri iliwakilishwa na Watendaji wa Kata na Vijiji, pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, walioungana na familia, ndugu, jamaa na wananchi katika maombolezo hayo.
Ushiriki huu si ishara ya upendo na mshikamano pekee, bali pia ni taswira ya utumishi unaozingatia kauli mbiu ya “Kazi na Utu”, ni utumishi unaothamini utu, mshikamano na kujali katika nyakati zote, ikiwemo wakati wa majonzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Ndugu Raymond Michael Mweli anaendelea kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watumishi wote wa Halmashauri hiyo, akiwataka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.







No comments:
Post a Comment