Na Mwandishi Wetu,Mbeya
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Mbeya,Rodrick Mpogole ameisihi jamii kuweka usawa katika malezi ya watoto wa kike na wa kiume ili kuwezesha makundi yote kupata haki sawa zikiwemo za ulizni na usalama kwenye maeneo yao.
Mpogole ametoa rai hiyo alipofungua mafunzo ya siku mbili ya Usafirishaji haramu wa binadamu na Uhamiaji salama yaliyoandaliwa na kwa ushirikiano baina ya Shirika la Community of Volunteers for the World(CVM) na Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi,Mahoteli,majumbani,huduma za jamii na ushauri(Chodawu)
Katika semina hiyo inayoratibiwa chini ya Mradi wa empowered II kwa ufadhili wa Serikali ya Italia kupitia Shirika la Italian Agency for Development Cooperation,Mpogole amesema katika siku za hivi karibuni jamii imeonekana kuwekeza nguvu zaidi kumtetea mtoto wa kike.
Amesema ni wakati kwa jamii kutambua kuwa watotyo wa kiume na wao wanapaswa kulindwa hasa kutokana na mmomonyoko wa maadili unaotokana na kukua kwa teknolojia inayosababisha wanajamii kuyajua mingi kupitia mitandao ya kijamii.
Amesema miongoni mwa vitendo vinavyochochea usafirishaji haramu wa binadamu ni pamoja na mapenzi ya jinsia moja ambapo kijana anaweza kujikuta ameangukia huko baada ya kulaghaiwa na wasafirishaji pasipo yeye kuujua ukweli.
“Leo watoto wa kiume ndiyo mashoga,hapa tunazungumzia habari ya usafirishaji haramu lakini wengine wakishachukuliwa ndiyo wanapelekwa kuwa mashoga.Sasa kupitia kikao hiki tutoke na jambo la kufanya kupambana na haya.Tuanzie kwenye mzizi.” Amesisitiza Mpogole
Katibu Tawala huyo amewataka wadau kuitumia Dira ya 2050 kama nyenzo ya kuweka usawa katika malezi hususani kaina eneo linalobainisha mwongozo wa malezi sawa kwa watoto wa kike na wa kiume tangu ngazi ya awali.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa empowered Mkoa wa Mbeya,Beltila Mligo amesema mafunzo hayo yamewalenga wadau mbalimbali wakiwemo viongozi tutoka taasisi zinazotakiwa kushirikiana katika kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu sambamba na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa majumbani.

No comments:
Post a Comment