Mmoja wa wanahabari washiriki wa mafunzo akichangia hoja.
Mwahabari mkongwe nchini Wence Mushi(Mbele) akiendelea kufundisha wana warsha katika hoteli ya Ruaha mjini Iringa.
Kutoka kulia ni wanahabari kutoka Mbeya Thompson Mpanji,Esther Macha na mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa wakifuatilia mafunzo yanayotolewa na Bw.Mushi.
HABARI KAMILI TOKA IRINGA
KUTOPEWA kipaumbele kwa ofisi za maafisa jamii na
maendeleo katika bajeti kumetajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayochangia kwa
kiasi kikubwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kuendelea kushamiri katika jamii.
Hayo yamebainishwa na wanahabari walioko kwenye
mafunzo ya masuala ya ukatili wa kijinsia yanayofanyika mkoani Iringa yakiwa
yameandaliwa na Chama cha waandishi wa habari wanawake(Tamwa) ambapo washiriki
wanatoka katika mikoa ya Mbeya,Iringa,Njombe na Ruvuma.
Wanahabari hao wamesema ofisi za maafisa ustawi wa
jamii zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa fedha kutokana na halmashauri
nyingi kutozipa kipaumbele ofisi hizo wakati wa upangaji wa bajeti.
Mmoja wa wanahabari hao Geofray Nihahi amesema wengi
wa maofisda kutoa ofisi hizo wamekuwa wakilalamika kukosa fedha na ndiyo sababu
hawatekelezi majukumu yao ipasavyo na badala yake wamebakia maofisini ambako
kimsingi hawana kazi zaidi ya kupiga soga.
Nihahi amesema uhaba huo wa fedha umesababisha
maafisa hao kushinda kutekeleza majukumu waliyopewa ikiwemo utoaji elimu kwa
jamii juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia hivyo kusababisha vitendo vya
ukatili kuendelea kukithiri.
Naye Cresensia Kapinga amesema ni wakati kwa wadau
wa masuala ya kijamii kujiuliza kwa kila mmoja ni kwa namna gani ameweza
kujitoa katika kuhakikisha anakomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye
jamii inayomzunguka na iwapo hajafanya basi atambue kuwa ana deni la kutekeleza
hayo.
Kwa upande wake Tumaini Msowoya,amesema bado katika
jamii kuna matukio mengi ya ukatili wa kijinsia na pia ukatili dhidi ya watoto
ambao baadhi ya wanajamii wanaufanya pasipo kujua kuwa wanakosea.




No comments:
Post a Comment