Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, June 30, 2014

HII INA TAFSIRI NINI,JE NI KUWAHADAA WAPIGA KURA KWAAJILI YA UCHAGUZI MKUU UJAO AU NI MAPENZI MEMA KWA WAPIGA KURA NA KUONESHA UCHUNGU KWA RASILIMALI ZA TAIFA??????/

Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akiwa katika usafiri wa Baiskeli akienda kutembelea wapiga kura wake kata ya Ifunda eneo la Kivalali wiki iliyopita ,kandop ni wananchi na viongozi wa kata hiyo. Mbunge Mgimwa akisalimiana na wanakikundi cha burudani Kivalali kata ya Ifunda SWALI LA MSINGI KWA WAPIGA KURA KUJIULIZA NI JE,HARAKATI HIZI ZA KUTETEA RASILIMALI ZA TAIFA KWA MBUNGE WAO KUFANYA ZIARA KWA KUTUMIA USAFIRI WA NAMNA HII ZITAKUWA ENDELEVU?NA JE KABLA KABLA YA UBUNGE ALIWAHI KUWATEMBELEA AKITUMIA USAFIRI WA AINA HII?NA JE IPO SIKU TUTAMUONA AKIENDA DODOMA KWA KUTUMIA USAFIRI HUU?

KWA HAYA SINA MANENO

Thursday, June 19, 2014

POLISI WAUA JAMBAZI,WAKAMATA SILAHA HATARI YA KIVITA

POLISI mkoani Mbeya wamemuua mtu mmoja anetuhumiwa kuwa ni jambazi na kufanikiwa kukamata bunduki ya kivita aina ya AK-47. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema tukio la kuuawa kwa mtuhumiwa wa ujambazi leo alfajiri katika mtaa wa Msikitini katika mji mdogo wa Tunduma uliopo wilayani Momba. Kamanda Msangi amesema baada ya polisi kuwatilia shaka watuhumiwa ambao walikuwa wawili waliamua kuwasimamisha lakini watuhumiwa hao walikaidi na kuanza kukimbia na baada ya kufika umbali wa mita chache mmoja kati yao akaanza kurusha risasi kuelekeza waliko askari. Amesema baada ya askari kuona hivyo waliamua kujibu na katika majibizano ya risasi jambazi mwenye silaha alipigwa risasi ubavuni na kufariki dunia papo hapo huku mwenzake akikimbilia kusikojulikana na anaendelea kutafutwa. Amesema baada ya kumuua jambazi huyo askari wamefanikiwa kukamata bunduki moja aina ya AK-47 yenye namba 592058 iliyokuwa na magazine yenye risasi 25 ukiacha tano alizokuwa amezifyatua awali. Baada ya kuupekua mwili wa marehemu pia polisi wamemkuta na kitambulisho cha mpiga kura chenye jina la Joseph Thadei Kapinga kinachoonyesha ni mkazi wa mtaa wa Mafiga katika manispaa ya Morogoro na alizaliwa tarehe 7.9.1971 Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

YATIMA ASHEREHEKEA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA MAJONZI

MTOTO Daudi Yisambi(9) mkazi wa kitongoji cha Sasyaka kijijini Masoko wilayani Mbeya hivi karibuni aliisherehekea siku ya Mtoto wa Afrika duniani kwa namna ya tofauti kwa yeye na familia yake kuwaomba wasamaria wema kumchangia fedha ili aweze kurejea hospitali kwaajili ya matibabu ya jeraha la moto lililomsababishia ulemavu. Mtoto Daudi ambaye ni Yatima aliyefiwa na wazazi wote wawili alipatwa na jeraha la moto baada ya kulipukiwa na petroli alipokuwa akicheza na watoto wenzake Oktoba mwaka jana nyuma ya mguu wake wa kulia usawa wa goti. Mtoto huyo ambaye hawezi kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili bali Kimalila pekee alisema alilipukiwa na petroli walipokuwa wakicchezea mafuta hayo na wenzake wakijua ni mafuta ya taa lakini baadaye akajikuta anapata jeraha kubwa. Alisema baada ya tukio hilo alipelekwa katika hospitali ya teule ya Ifisi iliyopo wilayani Mbeya ambako alitibiwa kwa takribani mwezi mmoja na kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata nafuu na alipewa dawa ya kuendelea kupaka katika jeraha lake. Alisema wakati akiendelea kuugua kidonda hicho akiwa anaishi nyumbani kwa bibi yake Mbushi Sendemle anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 75 na 80 ghafla mguu wake ulianza kujikunja kwa nyuma na hatimaye kidonda kikapona huku mguu ukishikamana kwa nyuma na sasa amepata ulemavu kwani hawezi tena kuunyoosha mguu huo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,kaka wa Daudi aliyejitambulisha kwa jina la Shila Yisambi ambaye wanachangia baba lakini mama tofauti na ambaye pia ni mlemavu wa kutoona jicho moja alisema walishindwa kumrudisha mdogo wake hospitali kutokana na kukosa fedha. “Ilikuwa vigumu kujua ni namna gani mdogo wangu aliungua na kupata jeraha kubwa katika mguu wake wa kulia kwani alikuwa akiishi na bibi yetu ambaye ni mzee sana.Baada ya matibabu ya awali pale Ifisi hatukuwa tena na fedha za kumrejesha hospitali.Pengine mdogo wangu asingepata ulemavu huu” alisema kaka wa Daudi. Kaka huyo alisema kwa sasa wanaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili waweze kumrejesha mdogo wake hospitali ili wataalamu waone uwezekano wa kumfanyia oparesheni mdogo wake ili ikiwezekana aepukane na ulemavu wa mguu huo kushikamana na aweze kutembea kama awali. Mtoto Daudi kwa hivi sasa analazimika kutembelea mguu mmoja unaosaidiana na mti jambo linaloonyesha kuwa tarayi amepata ulemavu kutokana na kukosekana kwa fedha za kumrejesha hospitali anakoweza kufanyiwa upasuaji na akaweza kutembea. Kutokana na ulemavu huo,hawezi kuvaa suruali hivyo hulazimika kushinda siku nzima akiwa amefunga kitenge kiunoni kwani ndilo vazi pekee linaloweza kuendana na umbile na ulemavu alionao kwa sasa. Mwenyekiti wa kitongoji cha Sisyaka Iyela Sisala alisema baada ya kuguswa na tatizo la mtoto huyo ikilinganishwa na uwezo mdogo wa kiuchumi alionao bibi yake na ndugu zakre wa karibu,wakazi wa kitongoji hicho waliamua kuanza kuchanga na hadi wakati akizungumza na mwandishi wetu jumla sha shilingi 60,000 zilikuwa zimechangwa. Lakini mwenyekiti huyo licha ya kusema michango ilikuwa ikiendelea kukusanywa,aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia kwa hali na mali kwa namna watakavyoguswa ili kuwezesha kumwokoa mtoto Daudi na ulemavu wa mguu. Afisa mradi wa Kupinga ukatili wa Kijinsia(UWAKI) na dhidi ya watoto(VAC) kupitia kanisa la Anglikana Patrick Cossima aliyepo pichani na mtoto Daudi baada ya hoja ya mtoto huyo kuwasilishwa katika sherehe za maadhimisho ya mtoto wa afrika katika kata ya Masoko licha ya kuchangia kiasi chya shilingi 30,000 aliahidi kufuatilia kwa karibu akishirikiana na wadau wengine ili kumwezesha mtoto huyo kurejeshwa hospitali na kufanyiwa upasuaji.

Tuesday, June 17, 2014

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA YAFANA KATIKA KATA ZA ILEMBO NA MASOKO

.WAELIMISHAJI WA MRADI WA KUPINGAA UKATILI WA KIJINSIA(GBV) NA UKATILI DHIDI YA WATOTO(VAC) WAKIONESHA MANJONJO KATIKA KUSAKATA MUZIKI . .Mmoja wa waelimishaji SINDE DASLAM AKISOMA RISALA MBELE YA MGENI RASMI NA WAGENI WAALIKWA Baadhi ya wakazi wa vijiji vya kata ya Masoko wilayani Mbeya wakisikiliza hotuba ya diwani wa kata hiyo Edward Mwampamba walipoungana na watoto wao katika sherehe za maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika

Sunday, June 15, 2014

DK.MWAKYEMBE AZINDUA COCACOLA BODABODA CUP 2014

Waziri wa Uchukuzi Dk.Harisin Mwakyembe akipiga penati kuzindua mashindano ya Cocacola Bodaboda Cup 2014 yanayofanyika jijini Mbeya yakishirikisha jumla ya timu kumi za madereva wa pikipiki za abiria maarufu kama Bodaboda.Ligi hiyo imemeandaliwa na kampuni ya City Sign Promotion and Marketing Argency ya jijini Mbeya. Dk.Mwakyembe akisalimiana na mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFA) Elias Mwanjala.Anayefuatia ni mlezi wa umoja wa waendesha na wamiliki bodaboda jijini Mbeya Nwaka Mwakisu .WAZIRI wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe,Jumamosi hii amezindua mashindano ya soka ya Coca Cola Bodaboda Cup 2014 yanayyoshirikisha jumla ya timu kumi za madereva wa bodaboda jijiji Mbeya. Akizindua mashindano hayo katika viwanja wa CCM Ilomba jijini Mbeya,Dk Mwakyembe amewataka waendesha boda boda hao kutumia mashindano kama njia ya kujikumbusha juu ya masuala muhimu ya usalama barabarani huku akipongeza wadau wa michezo mkoani hapa kwa kuleta mapinduzi katika michezo nchini. Amesema uwepo wa mikakati madhubuti baina ya wadau wa michezo mkoani hapa umewezesha kuibuka upya kwa amani,mshikamano na upendo baina ya wakazi na kusababisha mshikamano wa hali ya juu tofauti na miaka kadhaa iliyopita. Dk Mwakyembe pia aliwataka waratibu wa mashindano hayo kampuni ya City Sign Promotion and Marketing Agency kuwaalika wabunge wote wa mkoa wa Mbeya siku ya mchezo wa fainali ili kwa pamoja waweze kujionea namna michezo ilivyowezesha watu wa makundi yote kukutana na kuzungumza mambo ya msingi wakiweka tofauti zao pembeni. Awali mkurugenzi wa Habari na uenezi wa kampuni hiyo Geofray Mwangungulu alisema timu zinazoshiriki michuano hiyo zimegawanywa katika makundi mawili ya A na B ambapo kila kundi lina jumla ya timu tano na kila kundi litatoa timu mbili zitakazoingia hatua ya nusu fainali na baadaye kupatikana bingwa wa michuano. Kwa mujibu wa Mangunguru katika kundi A zipo timu za waendesha bodaboba za Mbalizi standi Umalila,Iyunga,Shewe Sae,Kadege na Uyole wakati kundi B zipo timu za Mbalizi standi Chunya,Ilomba,Soweto,Kabwe na Mafiati. Mwangungulu alisema bingwa wa mashindano hayo yatakayoendeshwa kwa muda wa siku 31 anatarajiwa kuzawadiwa pikipiki aina ya Boxer yenye thamani ya shilingi milioni 2.5,mshindi wa pili shilingi laki saba,mshindi wa tatu shilingi laki tatu na mfungaji bora shilingi laki moja.