HAYA NAYO YALIJIRI WAKATI WA MBIO ZA MWENGE MKOANI MBEYA
Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawilo aligomea kushusha bendera kwenye gari yake akitaka iendelee kupepea katika msafara wa Mbio za Mwenge wa Uhuru jambo ambalo ni kinyume kwakuwa hawezi kupeperusha bendera mbele ya kielelezo cha rais wake.Ililazimika kifanyike kikao kidogo cha dharula kati yake na wakimbiza mwenge kitaifa kama unavyoona hapo nyuma ya gari ya Mwenge.Kwa shingo upande ikambidi akubaliane kwakuwa msafara usingeendelea kama angeendelea na msimamo wa kupeperusha bendera katika gari yake hivyo iliondolewa na safari ikaendelea.
.Hiki nacho kilikuwa kituko kingine.Eti waratibu katika Jiji la Mbeya hawakujua kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa anaitwa nani mpaka wakaandika jina la mtu waliyekuwa wanamfahamu yeye.Mambo yalibainika asubuh mapema tu mara baada ya kuwekwa jiwe la msingi katika mradi wa kwanza na kiongozi wa Mbio za Mwenge akakuta jina si lakwake bali la mtu mwingine.Hapo ilibidi jiji wafanye utaratibu wa kumwagiza mtu katika miradi yote iliyofuata akaanze kuanzika upya jina la kiongozi wa mbio za mwenge.Unajua kilichotokea?Si ndio maandishi yakatofautiana na yale ya awali kama unavyoona katika hizo picha hapo juu.Siri ikawa hadharani.Hapo ilikuwa halmashauri ya nane tangu mkoa uingie katika mkoa wa Mbeya.Swali la kujiuliza ingekuwaje kama halmashauri hii ndiyo ingekuwa ya kwanza kuukimbiza Mwenge wa Uhuru?Hapa nadhani umakini ulikosekana.
Hapa ni Mbozi,Tanki hili la maji halijaanza kutumika bado,lakini hali ndiyo hii siku ya kuwekwa jiwe la msingi lina ubovu kwa kiasi hiki.Mamilioni ya walipa kodi yamepotelea.
No comments:
Post a Comment