Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, June 19, 2014

POLISI WAUA JAMBAZI,WAKAMATA SILAHA HATARI YA KIVITA

POLISI mkoani Mbeya wamemuua mtu mmoja anetuhumiwa kuwa ni jambazi na kufanikiwa kukamata bunduki ya kivita aina ya AK-47. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema tukio la kuuawa kwa mtuhumiwa wa ujambazi leo alfajiri katika mtaa wa Msikitini katika mji mdogo wa Tunduma uliopo wilayani Momba. Kamanda Msangi amesema baada ya polisi kuwatilia shaka watuhumiwa ambao walikuwa wawili waliamua kuwasimamisha lakini watuhumiwa hao walikaidi na kuanza kukimbia na baada ya kufika umbali wa mita chache mmoja kati yao akaanza kurusha risasi kuelekeza waliko askari. Amesema baada ya askari kuona hivyo waliamua kujibu na katika majibizano ya risasi jambazi mwenye silaha alipigwa risasi ubavuni na kufariki dunia papo hapo huku mwenzake akikimbilia kusikojulikana na anaendelea kutafutwa. Amesema baada ya kumuua jambazi huyo askari wamefanikiwa kukamata bunduki moja aina ya AK-47 yenye namba 592058 iliyokuwa na magazine yenye risasi 25 ukiacha tano alizokuwa amezifyatua awali. Baada ya kuupekua mwili wa marehemu pia polisi wamemkuta na kitambulisho cha mpiga kura chenye jina la Joseph Thadei Kapinga kinachoonyesha ni mkazi wa mtaa wa Mafiga katika manispaa ya Morogoro na alizaliwa tarehe 7.9.1971 Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment