Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, June 15, 2014

DK.MWAKYEMBE AZINDUA COCACOLA BODABODA CUP 2014

Waziri wa Uchukuzi Dk.Harisin Mwakyembe akipiga penati kuzindua mashindano ya Cocacola Bodaboda Cup 2014 yanayofanyika jijini Mbeya yakishirikisha jumla ya timu kumi za madereva wa pikipiki za abiria maarufu kama Bodaboda.Ligi hiyo imemeandaliwa na kampuni ya City Sign Promotion and Marketing Argency ya jijini Mbeya. Dk.Mwakyembe akisalimiana na mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFA) Elias Mwanjala.Anayefuatia ni mlezi wa umoja wa waendesha na wamiliki bodaboda jijini Mbeya Nwaka Mwakisu .WAZIRI wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe,Jumamosi hii amezindua mashindano ya soka ya Coca Cola Bodaboda Cup 2014 yanayyoshirikisha jumla ya timu kumi za madereva wa bodaboda jijiji Mbeya. Akizindua mashindano hayo katika viwanja wa CCM Ilomba jijini Mbeya,Dk Mwakyembe amewataka waendesha boda boda hao kutumia mashindano kama njia ya kujikumbusha juu ya masuala muhimu ya usalama barabarani huku akipongeza wadau wa michezo mkoani hapa kwa kuleta mapinduzi katika michezo nchini. Amesema uwepo wa mikakati madhubuti baina ya wadau wa michezo mkoani hapa umewezesha kuibuka upya kwa amani,mshikamano na upendo baina ya wakazi na kusababisha mshikamano wa hali ya juu tofauti na miaka kadhaa iliyopita. Dk Mwakyembe pia aliwataka waratibu wa mashindano hayo kampuni ya City Sign Promotion and Marketing Agency kuwaalika wabunge wote wa mkoa wa Mbeya siku ya mchezo wa fainali ili kwa pamoja waweze kujionea namna michezo ilivyowezesha watu wa makundi yote kukutana na kuzungumza mambo ya msingi wakiweka tofauti zao pembeni. Awali mkurugenzi wa Habari na uenezi wa kampuni hiyo Geofray Mwangungulu alisema timu zinazoshiriki michuano hiyo zimegawanywa katika makundi mawili ya A na B ambapo kila kundi lina jumla ya timu tano na kila kundi litatoa timu mbili zitakazoingia hatua ya nusu fainali na baadaye kupatikana bingwa wa michuano. Kwa mujibu wa Mangunguru katika kundi A zipo timu za waendesha bodaboba za Mbalizi standi Umalila,Iyunga,Shewe Sae,Kadege na Uyole wakati kundi B zipo timu za Mbalizi standi Chunya,Ilomba,Soweto,Kabwe na Mafiati. Mwangungulu alisema bingwa wa mashindano hayo yatakayoendeshwa kwa muda wa siku 31 anatarajiwa kuzawadiwa pikipiki aina ya Boxer yenye thamani ya shilingi milioni 2.5,mshindi wa pili shilingi laki saba,mshindi wa tatu shilingi laki tatu na mfungaji bora shilingi laki moja.

No comments:

Post a Comment