KIKAO CHA KUTOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA GBV NA VAC KATIKA KAMATI YA WILAYA YA MBEYA
Mwenyekiti wa kamati ya Kupinga Ukatili wa kijinsia(GBV) na ukatili dhidi ya watoto(VAC) wilani Mbeya Geofray Anania akizungumza jambo katika kikao kilichofanyika leo ndani ya ukumbu wa Youth Centre jijini Mbeya.Kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa mradi huo katika kata za Masoko na Ilembo unaoendeshwa na kanisa la Anglikana.
Mratibu wa mradi huo kutoka kanisa la Anglikana Mbeya Yona Mwakatobe akizungumza jambo kwenye kikao hicho.Baada ya afifa mradi Patrick Cossima kuwasilisha taarifa ya utekelezaji na wajumbe wa kikao kutoa hoja zao.
Mwanahabari Emmanuel Madafa(Kushoto) akifuatilia jambo kwa karibu na afisa mradi Patrick Cossima
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo kutoka ofisi ya Idara ya ustawi wa jamii akitoa mchango wake
Mwenyekiti wa kamati Geofray Anania akifunga kikao ambapo alisisitiza umuhimu wa wajumbe wa kamati kufanya ziara ya kutembelea kata za Masoko na Ilembo ili kujionea mazingira ya kata hizo na namna mradi wa GBV na VAC unavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zilizopo ili kuwa na mikakati ya pamoja ya mipango ya baadaye.
No comments:
Post a Comment