Na Mwandishi Wetu
KATIBU Tawala wa Wilaya
ya Mbeya, Mohamed Azizi leo amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Beno Malisa
kufungua Tamasha la Pre-Betika Mbeya Tulia Marathon 2026 lililofanyika ndani ya
Dimba la Sokoine
Kufanyika kwa Tamasha
hilo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea mashindano ya riadha ya Betika Mbeya
Tulia Marathon yatakayofanyika Mei 15-16 Mwaka huu ndani ya uwanja wa Sokoine
mkoani Mbeya kwa lengo la kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia jamii.
Azizi amesema anatamani
kuona mwaka huu mashindano hayo ya riadha yanashirikisha washiriki wengi zaidi
kutoka ndani na nje ya nchi na kuwataka wakazi jijini Mbeya hasa vijana kuchangamkia
fursa ya ujio wa wageni kufanya shughuli za kiuchumi.
“Wageni wengi watakuja
sasa ni wakati wa vijana kuchangamka,watakaouza vyakul,vinywaji,bodaboda
watasafirisha watu na nyumba za kulala wageni pia zitafanya biashara.”
Uzinduzi wa Pre-Betika Mbeya Tulia Marathon 2026 awali ulitanguliwa na mbio za pole(Joging) zilizoanzia eneo la Kituo kidogo cha mabasi cha Kabwe hadi Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya zikishirikisha vikundi mbalimbali vya mbio hizo.




No comments:
Post a Comment