Aliyewahi kuwa
mtangazaji wa Clouds FM,Couds TV na
Mjini FM,Barbara Hassan amewasihi wanafunzi kujenga tabia ya kusoma
vitabu kwa lengo la kujijenga kujiamini huku wakiamini kuwa Ndani ya Ndoto
Inawezekana.
Alitoa ujumbe huu
wakati wa kufanyika kwa mdahalo Iduda High School iliyopo Kkata ya Iduda Jimbo
la Uyole uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu kutoka ndani ya mkoa wa
Mbeya.
Mdahalo huo uliandaliwa
na Taasisi ya Tulia Trust ulikiwa na mada isemayo “Maisha kabla ya umaarufu na
safari ya mafanikio” huku kauli mbiu ikisema “Kutoka kuwa ndoto hadi uhalisia”*
huku wanafunzi wakihimizwa Kujifunza, kujiamini na kujitegemea.
No comments:
Post a Comment