Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (MNEC) Ndele Mwaselela amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 16 bora zinazoshiriki ligi ya Mama Samia Mshikamano Cup inayoendelea katika viunga vya wilaya hiyo, vifaa hivyo ni pamoja na mipira na jezi.Mwaselela amekabidhi vifaa hivyo vya michezo kwa timu 16 Julai 11, 2024 katika ofisi za CCM mkoa wa Mbeya.
Ametaka michezo ikawe chombo cha kuzitafsiri 4R za Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuelezwa kwa mambo makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya utawala wa rais huyo.



No comments:
Post a Comment