Mabingwa wa Tanzania Bara wako Afrika kusini ambapo leo majira ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania watashuka uwanja wa Mbombela huko Mpumalanga kuikabili Augsburg Fc katika mchezo wa ufunguzi michuano ya Mpumalanga International Cup
Huo utakuwa mchezo wa kwanza wa pre-season kwa kocha Miguel Gamondi na kikosi chake kilichoanza maandalizi Julai 08 pale Avic Town
Ukimuondoa Pacome Zouzoua nyota wote waliosafiri Afrika Kusini na kikosi cha Yanga wako tayari kwa mchezo huo
Suala la Pacome lilitolewa ufafanuzi na Yanga ambapo nyota huyo alipewa ruhusa ya kurejea kwao Ivory Coast kushughulikia masuala ya kifamilia. Pacome ataungana na Yanga Julai 24 huko huko Afrika Kusini
Pamoja na kuwa ni mechi ya pre-season, nyota wa Yanga wamepania kuonyesha uwezo wao mbele ya wajukuu hao wa Hitler
Itakuwa heshima kubwa kama Yanga wataibuka na ushindi dhidi ya timu inayoshiriki Bundesliga
Je unadhani ushindi wa Yanga leo utawapelekea salamu wengine wafahamu kuwa msimu huu Yanga ina jambo lake Kimataifa?

No comments:
Post a Comment