Kile ambacho Yanga walikifanya kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu uliopita walipokwenda Rwanda kucheza na Al Merrikh wamepanga kurudia tena watakapokwenda Burundi kumenyana na Vital'o katika hatua ya awali ya michuano hiyo msimu huu
Meneja wa habari na mawasiliano Ali Kamwe amesema watafanya kampeni kubwa kuhakikisha Mashabiki wanakwenda kwa wingi Burundi kama walivyofanya msimu uliopita walivyokwenda rwanda
'Droo tumeiona na tumefurahi sana kwani tutahakikisha tunakwenda kuweka rekodi Burundi kama tulivyofanya Rwanda kucheza na Al Merrikh"
"Maandalizi yetu yanaendelea vyema Avic Town, huu ni msimu mwingine ambao tumeweka malengo ya kufanya vizuri zaidi. Ni mechi za mtoano ambazo hupaswi kumdharau mpinzani wako"
"Akili yetu sasa inaziwaza dakika 180 hizi dhidi ya Vital'o tukishamaliza ndio tutaanza kuangalia mchezo unaofuata utakuwaje," alisema Kamwe
Kama Yanga utavuka hatua ya awali raundi ya kwanza itachuana na mshindi wa mchezo kati ya SC Villa ya Uganda naCommercial Sports ya Ethiopia

No comments:
Post a Comment