“Nimejisikia furaha kwa sababu nimekuja katika timbu ambayo
nilikuwa naiota, nimekuwa naiwaza siku zote kwa hiyo nimefurahi kukutana na
wenzangu. Wenzangu wamenipokea vizuri na nimejiandaa kwaajili ya kuipambania
timu yangu”
Ni maneno ya mchezaji 'kiungo fundi wa mpira' Awesu Ally Awesu akiwa
mazoezini kwa mara ya kwanza na kikosi cha wekundu wa msimbazi baada ya kutua nchini
Misri.
Hatiamaye ametimiza ndoto ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Miamba wa Soka Nchini na Afrika Simba SC marehemu Zacharia Hans
Poppe ya kumuona akikipiga kunako wekundu wa Msimbazi, Simba Sc.
Ni jicho la ziada la kutambua
vipaji la Hans Pope ndilo lililomuibua kwa mara ya kwanza Awesu Awesu. Aliwahi
kuitwa Rasta wa Hans Poppe kutokana na utambulisho wake mkubwa wa mtindo wa
nywele.
Ilikuwa kwenye nusu fainali ya FA kati ya Madini SC dhidi ya Simba SC katika dimba la Sheikh Amri
Abeid wa jijini Arusha uliopigwa mwaka 2017. Awesu Awesu akichezea Madini ya
Arusha katika pambano lile alikiwasha na kuisumbua sana safu ya kiungo ya
Simba.
Ndipo jicho la Zacharia Hans Poppe lilipomuona kijana mwenye
Rasta ambaye aliisumbua kweli kweli
Simba. Katika pambano hilo Simba walishinda kwa taabu 1-0.
Baada ya pambano lile Hans Poppe alipiga picha ya ukumbusho na
Uwesu Awesu na kuzungumza naye mambo machache na inawezekana kubwa kabisa ni
hapo baadaye atue Msimbazi
Ni baada ya miaka nane sasa Awesu Awesu ametua Msimbazi na yupo
kambini Misri akijiwinda kwa msimu ujao wa mashindano mbalimbalj ikiwemo Ligi
kuu ya NBC.
Akiwa Misri Awesu Awesu amekaririwa akieleza furaha yake ya
kutimia kwa ndoto yake ya kutua katika timu ya moyo wake.



No comments:
Post a Comment