Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, November 16, 2024

TYSON AAMBULIA KICHAPO


Jake Paul amemshinda bondia nguli Mike Tyson kupitia uamuzi wa Pamoja katika mpambano wa uzito wa juu uliofanyika Texas Marekani. Pigano kati ya Paul, mtengeneza maudhui mwenye umri wa miaka 27 na Tyson, bingwa wa zamani wa uzito wa juu mwenye umri wa miaka 58, halikuwaridhisha mashabiki.

Mkongwe Tyson hakuweza kuonesha makali dhidi ya mpinzani wake huyo chipukizi. Tyson alimrushia ngumi 18 tu wakati Paul akimnyeshea nvua ya ngumi 78. Pigano hilo lilienda raundi zote nane. Jaji mmoja alimpa Paul pointi 80 dhidi ya 72 wakati wengine wawili wakimpa pointi 79-73.

"Kwanza kabisa, Mike Tyson – ni heshima kupambana naye ulingoni," alisema Paul. Mike, yeye ni mkongwe, nimetiwa moyo naye, na tusingekuwa hapa leo bila yeye.”

Naye Tyson baada ya kichapo alisema, “Nilijua ni bondia mzuri. Alikuwa amejiandaa. Nilikuja kupigana. Sikumdhihirishia yeyote kitu, ila mimi mwenyewe.”

Kwa hisani ya DW

ANASEMA KOCHA MPYA WA YANGA

 


Friday, November 15, 2024

KAMANDA KUZAGA ATOA SOMO KWA WANAVYUO MBEYA AKIFUNGUA DREAMS INTERCOLLEGE



Na Mwandishi Wetu

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amewataka wanavyuo mkoani Mbeya kujiepusha na vitendo visivyofaa katika jamii ikiwemo uhalifu.

Hayo ameyasema Novemba 14, 2024 wakati akifungua mashindano ya mpira wa miguu yanayohusisha vyuo vikuu mkoani humo yanayojulikana kama "Dreams Intercollege" yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya.
Kamanda Kuzaga amewataka wanavyuo mkoani humo kuyatumia mashindano hayo kama sehemu ya kujenga upendo, umoja, mshikamano na kufahamiana kati ya chuo na chuo na wanavyuo na sio uadui.
Aliongeza kuwa, mashindano hayo yakawe chachu katika kuibua vipaji vya mpira wa miguu kwa wanavyuo mkoani humo kwani michezo ni ajira hivyo alisisitiza kutumia vizuri fursa ya kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Naye, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mbeya Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Veronica Ponera amewataka wanavyuo mkoani humo kujiepusha na ukatili wa kijinsia, kujiepusha na tamaa ya vitu vya thamani ambavyo vinaweza kuwaingiza kwenye vishawishi vya vitendo viovu.
"Jeshi la Polisi nchini linaendelea na kampeni ya Tuwaambie kabla hawajaharibiwa hivyo ni nafasi kwetu kuwaeleza wanavyuo mambo ya kujiepusha nayo kabla hamjaharibikiwa na kupoteza dira ya kufikia ndoto zenu" alisema ASP Ponera.
Awali akizungumza Mratibu wa mashindano hayo Meneja wa kituo cha redio"Dreams fm" cha Jijini Mbeya ndugu Samuel Mhina amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha wanavyuo wote waliopo mkoani Mbeya, T.I.A ambaye ni bingwa mtetezi, CUoM, Tumaini, MUST, Chuo cha Afya - Ifisi yakiwa na lengo la kujenga umoja na kuibua vipaji.
Mechi ya ufunguzi ambayo iliwakutanisha chuo kikuu cha katoliki Mbeya (CUoM) dhidi ya T.I.A imemalizika kwa kushuhudia CUoM ikiibuka na ushindi wa magoli matano kwa bila na kukabidhiwa ngao ya jamii ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mashindano hayo.

YANGA YAACHANA RASMI NA GAMOND


Uongozi wa klabu ya Yanga Sc umethibitisha kuvunja mkataba na kocha wa kikosi cha kwanza Miguel Angel Gamondi raia wa Argentina pamoja na kocha msaidizi Moussa Ndaw.

Taarifa ya leo Novemba 15, 2024 iliyotolewa na klabu hiyo imebainisha kuwa klabu hiyo tayari imeanza mchakato wa haraka wa kutafuta Makocha wapya wa kikosi hicho na unatarajiwa kukamilika hivi punde.
“Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuwashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya.” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Thursday, November 14, 2024

KING KIKII AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Boniface Kikumbi maarufu King Kikii amefariki dunia.

Mwanamuziki huyo ambaye ameugua kwa muda mrefu, amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 15 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu

Marehemu King Kikii atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Kwa miaka mingi ameburudisha, amefundisha na kuelimisha jamii kupitia nyimbo zake.

Enzi za uhai wake,Marehemu King Kikiii alitamba na vibao mbalimbali kikiwemo cha 'Kitambaa cheupe'.

King Kikii alikuwa Mtunzi na mwimbaji wa zamani wa Marquiz du Zaire na Orchestra Double O ambaye pia alikuwa mmiliki wa bendi ya La Capital, inayotesa na mtindo wake wa Kitambaa Cheupe

Alizaliwa mwaka 1947 katika Jiji la Lubumbashi lililopo kwenye Mkoa wa Katanga, eneo maarufu huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC)

Saturday, October 12, 2024

TULIA STREET TALENT COMPETITION 2024 MSIMU WA TANO KUFANYIKA OKTOBA 25-28,2024

 

Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya Tamasha la Kuibua vipaji.


Tamasha la kuibua vipaji vya kucheza(Dance),mitindo(Fashion),kuchekesha(Comedy) na Dj Mixing lililoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust litafanyika Oktoba 25-28,2024 katika uwanja wa Chuo cha Uhasibu(TIA) jijini Mbeya.

Akitoa taarifa kwa wanahabari Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo amesema tamasha hilo ni la tano kufanyika ambalo litajumuisha washiriki kutoka nchi nzima. 

“Fomu zimeanza kutolewa Oktoba 9,2024 hadi Oktoba 20,2024 saa 9:30 alasili katika ofisi za Tulia Trust zilizopo Uyole jijini Mbeya, Tukuyu wilayani Rungwe na Kyela. 

Sifa za mshiriki awe ni Mtanzania yeyote mwenye kipaji Mawasiliano namba 0657389521 na 0769060738. 

Mshindi wa kuimba atarekodi nyimbo katika studio ya Black Dot Music iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Wednesday, August 14, 2024

DC RUNGWE ATAKA MADIWANI KUKEMEA UKATILI DHIDI YA ALBINO, WATOTO


Na Mwandishi Wetu, Rungwe

MADIWANI katika Halimashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vya mauaji dhidi ya watu wenye ualbino pamoja na ukatili dhidi ya watoto.

 

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu alisisitiza hilo alipotoa salamu za serikali kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/24.

 

Haniu alisema katika maeneo mbalimbali nchini kumeanza kuonekana matukio ya mauaji dhidi ya watu walio na ualbino matukio aliyosema yamekuwa yakiibuka nyakati za kuelekea chaguzi hatua aliyosema ni imani zisizopaswa kupewa nafasi kwakuwa hakuna uhusiano kati ya uchaguzi na ualbino.

Sunday, July 28, 2024

JEZI MPYA YANGA 2024/25

 




ALICHOKIANDIKA MWANASHERIA WA YANGA


"Hizi changamoto za wachezaji wenye mikataba kutoroka timu zao ni matokeo ya ushabiki na wachambuzi wetu"

"Kwa sasa, kuna wimbi la wachezaji kutoroka na wengine kuwa na mikataba na timu zaidi ya moja kwa madai kwamba hawana furaha na wanaenda kutafuta fursa bora zaidi"
"Ushauri wangu kwa BMT ili kuokoa soka letu ni kuweka kanuni inayolazimisha mchezaji yeyote mwenye mkataba akihama kutoka klabu moja kwenda nyingine lazima kuwe na Mkataba wa Uhamisho (Transfer Agreement) au Mkataba wa Kusitisha kwa Pamoja (Mutual Termination Agreement) uliothibitishwa na BMT na kulipiwa ushuru wa stampu (Stamp Duty)"
"Mchezaji au timu yoyote ikikiuka, basi mchezaji huyo asipewe kibali cha kucheza nchini, periodt."
"Bila hatua hiyo, migogoro ya wachezaji wenye mikataba haitaisha kamwe na TFF itaendelea kulalamikiwa bure."
"NB: Kwakuwa tulishakubaliana kama mchezaji hana furaha aruhusiwe kuondoka, Rasta asiguswe acha ale maisha
😂
" Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga SC, Simon Patrick.

MILIONI 10 KUKARABATI UWANJA WA SOKOINE




Na Lyamba Lya Mfipa

SHILINGI milioni kumi zinatarajiwa kutumika kwaajili ya ukarabati wa Uwanja wa Kumbumbu ya Sokoine lengo likiwa ni kuuweka kweny hadhi stahiki ya kutumiwa kwa mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi kuu ya Tanzania bara.

 

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Mbeya, Langaeli Akyoo alisema kuwa maboresho yanayofanyika ni pamoja na kupaka rangi kwenye viti vya kukalia mashabiki, kufunga seng'enge mpya na kujenga vibanda vipya vya benchi la ufundi.

 

Akyoo alisema ukarabati huo ni utekelezaji wa maelekezo ya  barua waliyopokea kutoka Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ya kuwataka wamiliki hao kufanya maboresho kadhaa katika uwanja huo ili kuendana na viwango vinavyohitajika.

 

"Tulipokea barua kutoka TFF ikitutaka, kufanya ukarabati na maboresho kadhaa, ikiwemo kupaka rangi viti vinavyokaliwa na mashabiki, kufunga seng'enge vizuri kuzunguka uwanja na kujenga upya vibanda vinavyokaliwa na benchi la ufundi, na tayari zoezi hili tunaendelea nalo" alisema Akyoo

 

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge, akiwa ameongozana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (M-NEC), Ndele Jailos Mwaselela na Katibu Mwenezi Christopher Uhagile jana walifika uwanjani hapo kukagua maendeleo ya ukarabati huo unaoendelea.

 

Akiwa eneo la tukio Mwalunenge alisema kuwa wametenga zaidi ya shilingi milioni 10 ambazo zitatumika kupaka rangi kuzunguka uwanja, na kudai kuwa mpango uliopo ni kufanya ukarabati mkubwa ikiwa ni pamoja na kujenga majukwaa ya mashabiki ili wasilowe na mvua pia kujenga vibanda vya kisasa vya kufanyia biashara kuzunguka uwanja.

 

"Mpango wetu ni kuufanya uwanja wetu uvutie zaidi, kwahiyo tunaendelea kutafuta wadau mbalimbali watakao tuunga mkono ili tufanye maboresho makubwa sana kwenye uwanja wetu huu,  tutajenga majukwaa kuzunguka uwanja hata kama mvua inanyesha mashabiki wasilowe, pia tuna mpango wa kufunga taa ili mpira uchezwe hata nyakati za usiku" alisema Mwalunenge

 

Kwaupande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (M-NEC), Ndele Mwaselela alimpongeza Mwenyekiti Mwalunenge kwa jitihada hizo,  kwa madai kuwa kazi hizi za kujitolea zinahitaji zaidi moyo wa kujitoa.

 

Meneja wa uwanja Modestus Mwaluka alisema rangi inayopakwa uwanjani hapo ni ya kijani na njano na kueleza kuwa mkandarasi aliyepewa kazi hiyo anatarajia kukamilisha kazi hiyo ndani ya siku saba.

Yanga SC vs Kaizer Chiefs Toyota Cup leo


 LEO, wananchi Yanga SC watakuwa dimbani kucheza na Kaizer Chiefs ni katika Kombe la Toyota


Mechi hii itapigwa kuanzia saa 10:00 jioni na kuruka mbashara AzamSports1HD

Ni pira Nabi ama pira Gamondi lipi kuondoka na ushindi?

Thursday, July 25, 2024

YANGA YAPATA MTEREMKO

 


Mabingwa wa ligi kuu nchini Burundi Vital'o wanatarajiwa kutumia uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Yanga

Vital'o wamelazimika kuleta mchezo huo Dar kwakuwa Burundi haina uwanja uliokidhi matakwa ya CAF kwaajili ya michuano hiyo
Ni wazi sasa Yanga haitasafiri nje ya Tanzania katika mechi zake za hatua ya awali zitakazopigwa August 16-18 na August 24-26
Yanga inatarajiwa kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi ya mkondo wa pili
Msimu huu Yanga imeweka malengo makubwa katika michuano ya ligi ya mabingwa ambapo Wananchi wanautaka ubingwa wa Afrika

Sunday, July 21, 2024

Kitengo cha habari cha Young Africans SC ya Tanzania na Kitengo cha habari cha FC Augsburg ya Ujerumani kwenye picha ya pamoja

 


AL HILAL RASMI MSHINDI WA TATU DARPORT KAGAME CUP 2024

 



Al Hilal rasmi amechukua nafasi ya Mshindi wa Tatu wa Michuano ya Darport Kagame Cup 2024 baada ya mikwaju ya penati 3-2. Hii ni baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1 katika uwanja wa KMC Stadium.

RASTA WA HANS POPPE AFURAHIA KUTUA MSIMBAZI

 

 Na Mwandishi Wetu.

“Nimejisikia furaha kwa sababu nimekuja katika timbu ambayo nilikuwa naiota, nimekuwa naiwaza siku zote kwa hiyo nimefurahi kukutana na wenzangu. Wenzangu wamenipokea vizuri na nimejiandaa kwaajili ya kuipambania timu yangu”

 

Ni maneno ya mchezaji 'kiungo fundi wa mpira' Awesu Ally Awesu akiwa mazoezini kwa mara ya kwanza na kikosi cha wekundu wa msimbazi baada ya kutua nchini Misri.

 

Hatiamaye ametimiza ndoto ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Miamba wa Soka Nchini na Afrika Simba SC marehemu Zacharia Hans Poppe ya kumuona akikipiga kunako wekundu wa Msimbazi, Simba Sc.

 

Ni jicho la ziada la kutambua  vipaji la Hans Pope ndilo lililomuibua kwa mara ya kwanza Awesu Awesu. Aliwahi kuitwa Rasta wa Hans Poppe kutokana na utambulisho wake mkubwa wa mtindo wa nywele.

 

Ilikuwa kwenye nusu fainali ya FA kati ya Madini SC  dhidi ya Simba SC katika dimba la Sheikh Amri Abeid wa jijini Arusha uliopigwa mwaka 2017. Awesu Awesu akichezea Madini ya Arusha katika pambano lile alikiwasha na kuisumbua sana safu ya kiungo ya Simba.

 

Ndipo jicho la Zacharia Hans Poppe lilipomuona kijana mwenye Rasta ambaye aliisumbua  kweli kweli Simba. Katika pambano hilo Simba walishinda kwa taabu 1-0.

 

Baada ya pambano lile Hans Poppe alipiga picha ya ukumbusho na Uwesu Awesu na kuzungumza naye mambo machache na inawezekana kubwa kabisa ni hapo baadaye atue Msimbazi

 

Ni baada ya miaka nane sasa Awesu Awesu ametua Msimbazi na yupo kambini Misri akijiwinda kwa msimu ujao wa mashindano mbalimbalj ikiwemo Ligi kuu ya NBC.

 

Akiwa Misri Awesu Awesu amekaririwa akieleza furaha yake ya kutimia kwa ndoto yake ya kutua katika timu ya moyo wake.

Saturday, July 20, 2024

Augsburg 2 - 1 Yanga

 






BAADA ya mechi kati ya Yanga SC 
🇹🇿 dhidi ya Augsburg ðŸ‡©ðŸ‡ª kumalizika beki wa Klabu ya Augsburg ðŸ‡©ðŸ‡ª ambaye pia ndiye mfungaji wa goli la kwanza La Augsburg, Mady Pedersen alimfuata kwenye Dressing Room Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Maxi Nzengeli akampongeza kisha wakabadirishana jezi.

Maxi Nzengeli ndiye aliyetoa pasi ya goli lililofungwa na Mshambuliaji Jean Baleke.

Vikosi vya YANGA SC na AUGSBURG

 



Ni Yanga na Augsburg saa 10 leo


Mabingwa wa Tanzania Bara wako Afrika kusini ambapo leo majira ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania watashuka uwanja wa Mbombela huko Mpumalanga kuikabili Augsburg Fc katika mchezo wa ufunguzi michuano ya Mpumalanga International Cup

Hii ni michuano maalum ya pre-season inayoshirisha timu nne, Yanga na Augsburg inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga) ni timu zilizoalikwa
Huo utakuwa mchezo wa kwanza wa pre-season kwa kocha Miguel Gamondi na kikosi chake kilichoanza maandalizi Julai 08 pale Avic Town
Ukimuondoa Pacome Zouzoua nyota wote waliosafiri Afrika Kusini na kikosi cha Yanga wako tayari kwa mchezo huo
Suala la Pacome lilitolewa ufafanuzi na Yanga ambapo nyota huyo alipewa ruhusa ya kurejea kwao Ivory Coast kushughulikia masuala ya kifamilia. Pacome ataungana na Yanga Julai 24 huko huko Afrika Kusini
Pamoja na kuwa ni mechi ya pre-season, nyota wa Yanga wamepania kuonyesha uwezo wao mbele ya wajukuu hao wa Hitler
Itakuwa heshima kubwa kama Yanga wataibuka na ushindi dhidi ya timu inayoshiriki Bundesliga
Je unadhani ushindi wa Yanga leo utawapelekea salamu wengine wafahamu kuwa msimu huu Yanga ina jambo lake Kimataifa?

Friday, July 19, 2024

ASILI YA WAPOGOLO

 


Wapogolo ni kabila la watu kutoka kusini-kati ya nchi ya Tanzania, hususanI Mkoa wa Morogoro. Lugha yao ni Kipogolo.

Mwaka 1987 idadi ya Wapogolo ilikadiriwa kuwa 185,000
Historia
Inasemekana asili yao ni Afrika Magharibi, hasa katika nchi ya Senegal, pia Afrika ya Kati Congo. Kuna mila nyingi Senegal na ngoma zake nyingi zinafanana na Sangula. Sababu ya kuhamia Tanzania ilikuwa utafutaji wa ardhi ya kilimo na mabadiliko ya hali ya hewa. Waliendelea kuhama zaidi kutoka Senegal na wengine walikimbilia pia Zambia, Zimbabwe na Malawi. Ndiyo maana kuna ukoo mkubwa wa Matimba kule Malawi na huko Zimbabwe.

Tuesday, July 16, 2024

LIGI KUU YA NBC 2024/25 KUANZA AGOSTI 16

 


Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara TPLB imetangaza Agosti 16 kuwa tarehe rasmi ya kuanza kwa ligi kuu ya NBC 2024-2025

Yanga SC ndiyo mabingwa watetezi wa ligi hiyo wataungana na klabu nyingine 15 kukamilisha klabu 16 ambazo zitashiriki ligi katika msimu mpya wa mashindano
Wakati klabu mbalimbali zikijiandaa kumaliza katika nafasi nne za juu, Kengold FC kutoka Chunya Mbeya na Pamba Jiji FC kutoka Mwanza zitaingia katika ligi hiyo kama wageni baada ya kufanikiwa kupanda daraja msimu huu.

Sunday, July 14, 2024

UJUE USAJIRI WA SIMBA 2024/25

 


Wachezaji (18) walioondoka Simba SC 2024/25

1. Aishi Manula (Azam FC)
2. Feruz (Loan)
3. David Kameta 'Duchu' (Loan)
4. Hussein Kazi (Loan)
5. Clatous Chama (Yanga SC)
6. Abdallah Hamiss.
7. Aubin Kramo.
8. Babakar Sar.
9. Sadio Kanoute
10. Moses Phiri.
11. Luis Miquissone.
12. Pa Omary Jobe.
13. Willy Esomba Onana.
14. Hennock Inonga.
15. Saido Ntibazonkiza.
16. John Bocco.
17. Jimmyson Mwanuke.
18. Shaban Chilunda.
19. Kennedy Juma.
Wachezaji (13) waliosajiliwa Simba SC 2024/25
1. Lameck Lawi (⚠️)
2. Joshua Mutale.
3. Steven Mukwala.
4. Jean Charles Ahoua.
5. Abdulrazack Hamza.
6. Debora Mavambo.
7. Augustine Okejepha.
8. Omary Abdallah Omary.
9. Valentine Nouma.
10. Valentino Mashaka.
11. Chamou Karaboue.
12. Yusuph Kagoma.
13. Kelvin Kijili.
Wachezaji wa kigeni wa Simba SC 24/25
1. Ayoub Lakred 🇲🇦
2. Chamou Karaboue 🇨🇮
3. Che Fondoh Malone.
4. Valentine Nouma 🇧🇫
5. Fabrice Ngoma 🇨🇩
6. Debora Mavambo 🇨🇬
7. Augustine Okejepha 🇳🇬
8. Freddy Michael 🇨🇮
9. Joshua Mutale 🇿🇲
10. Steven Mukwala 🇺🇬
11. Jean Charles Ahoua 🇨🇮